KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, January 9, 2015

RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU 201 KWA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI, AAGANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA RWANDA.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe Ali Siwa, Balozi wa
Tanzania nchini Rwanda aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam, kuaga rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye kituo
chake cha kazi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe Jacky Zoka, Balozi
wa Tanzania nchini Canada aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam, kuaga rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye
kituo chake cha kazi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Mhe Jacky Zoka, Balozi wa
Tanzania nchini Canada na Mhe Ali Siwa, Balozi wa Tanzania nchini
Rwanda,  walipofika  Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9,
2015   kuaga rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya
kazi.

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza   Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  alipokuwa akimjshukuru kwa
kutoa vitabu 2752 kwa Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za  JWTZ
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya
Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC)  iliyofanyika Ikulu
jijini Dar es salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya
vitabu   na  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Kikwete
amekabidhi  vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi
(National Defence College - NDC)  iliyofanyika Ikulu jijini Dar es
salaam.Rais kikwete, ambaye ameshachangia
jumla ya vitabu 2752 katika  maktaba ya chuo hicho na chuo cha Monduli
katika vipindi tofati,  amesema elimu imo vitabuni, na ili kuelemika
yapaswa mtu asome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa
na vitabu.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na   Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ baada
ya  hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo
cha Ulinzi (National Defence College - NDC)  iliyofanyika Ikulu jijini
Dar es salaam.(PICHA NA IKULU)

No comments: