Ndegevita
za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita
moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa
kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita
za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali
akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na
kusababisha ndegevita kuwaka moto.
Hata
hivyo, rubani wa ndgevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa
kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa
maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa
hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .
Wananchi
wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na
kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala
miundo mbinu.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari
na Mahusiano
Makao Makuu ya
Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano
zaidi: 0783-309963
No comments:
Post a Comment