Baadhi ya washiriki wa mkutano
maalum wa watendaji wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na
Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia masuala mbalimbali.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufungua mkutano maalum wa watendaji wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na
Wafanyakazi (TUCTA).
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) jijini Dar es salaam. Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali
zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi nchini.
Baadhi ya washiriki wa mkutano
maalum wa watendaji wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na
Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia masuala mbalimbali.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza jambo na Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila kabla ya kuanza kwa mkutano maalum wa watendaji wa
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa –
MAELEZO
Dar es
salaam.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila ametoa wito kwa watendaji wa Mahakama
Kuu Divisheni ya Kazi nchini kufanya kazi
kwa kuzingatia weledi, viwango na uadilifu ili mahakama hiyo iendelee kuwa
kimbilio la wananchi wanaotafuta haki.
Akizungmza wakati wa
wakati wa kikao cha wadau wa Mahakama kujadili uboreshaji wa utendaji kazi
katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kilichowahusisha watendaji wa Mahakama ya
Kazi , Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) leo jijini Dar es slaam, Mhe.Shaaban Lila amesema kuwa msingi mkuu wa Mahakama ya Tanzania nikuhakikisha
kuwa inatoa maamuzi kwa wananchi kwa haki na wakati.
Amesema iwapo waajiri na waajiriwa kote nchini haki
watazingatia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao kulingana na kanuni na
taratibu zinazosimamia maeneo ya kazi migogoro
mingi inayopelekwa mahakamani baina ya waajiri na waajiriwa itapungua
nchini.
“Kila upande ifanye kazi yake kwa haki
,kumekuwa na mrundikano wa mashauri ya
kazi yanayokwenda mahakamani kwa ajiri ya utatuzi na usuluhishi ,mengi ya
mashauri hayo hayahusiani na kufukuzwa kazi isipokuwa yale ya kukosa uaminifu,
wizi na ubadhirifu sehemu za kazi” Amesisitiza.
Amebainisha kuwa
Mahakama ya Tanzania lazima iheshimiwe kutokana na misingi yake kwa kuweka
msisitizo katika kushughulikia masuala ya msingi na kutatua kero za wananchi
hususan usimamizi na utoaji wa haki kwa wakati.
Mhe. Shaaban amefafanua
kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya maboresho na mabadiliko katika
kushughulikia mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani huku akieleza kuwa mkakati
wa sasa ni kupunguza umri wa mashauri ya muda mrefu ya miaka 5 hadi 10 yanayofikia
265 na yale ya umri wa miaka 3 yapatayo
201 yaweze kushughulikiwa ndani ya mwaka 1 hadi 2 ifikapo June 2015.
“Lengo letu ni
kushughulikia mashauri haya haraka kwa muda mfupi, muhakikishe mashauri haya
mnayamaliza kwa sababu yanagusa uzalishaji na maisha ya watu, kuchelewa kuyasikiliza
kunaathiri uchumi ” Amesisitiza.
Aidha,amewataka wadau wanaoshiriki
mkutano huo kujipima katika malengo wanayojiwekea pamoja na kusimamia
utekelezaji wa hukumu na maamuzi yanayotolewa na mahakama na kueleza kuwa ofisi
yake inaandaa mkakati wa usimamizi wa suala hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
Waajiri nchini Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mulimuka akizungumza katika mahojiano
maalum amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwaweka pamoja wadau hao kwa maana ya Mahakama, Waajiri (Serikali)
na waajiriwa unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali
zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi nchini.
Amesema asilimia 70 ya
mashauri yanayokwenda mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi yanahusu migogoro ya waajiri
kuwasimamisha kazi wafanyakazi wao kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa mengi ya makosa hayo hayasababishi mtu
afukuzwe kazi.
Ametoa wito kwa pande
zote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kufuata haki ili mashauri
yote yanayopelekwa mahakamani yaweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuondoa
migogoro ya kazi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment