KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, February 4, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AMPOKEA MKE WA RAIS WA JAMHURI YA UJERUMANI MAMA DANIELLA SCHADT.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha Ikulu Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova kwenye viwanja vya Ikulu.
 Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea salamu ya heshima mara baada ya mgeni huyo kuwasili Ikulu akiwa kwenye ziara ya kiserikali hapa nchini.
 Rais Jakaya Kikwete na Mke wake Mama Salma wakiandamana na wageni wao Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Mke wake Schadt wakingia Ikulu huku mamia ya wananchi wakishangilia kwa furaha huku wakipeperusha bendera za hizo nchi mbili.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, wakati mgeni huyo alipowasili kwenye ofisi hizo akiambatana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Daniella Schadt wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya WAMA, Mama Hulda Kibacha (kushoto) na Blandina Nyoni (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea ofisi hiyo.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akiweka saini yake kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za WAMA akiambatana na mwenyeji wake Mama Salma Kikwete.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi Jarida la WAMA kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt wakati alipotembelea ofisi za WAMA.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Schadt zawadi ya kanga.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Schadt zawadi ya kanga.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt kwenye ofisi za WAMA.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt akiagana na wajumbe wa bodi ya WAMA pamoja na wafanyakazi mara baada ya kutembelea ofisi hizo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Scahdt wakimwangalia mgonjwa Kundi Girogui aliyetoka wilaya ya Serengeti ambaye aliyefanyiwa upasuaji wa mdomo kwenye hospitali ya CCBRT huko Msasani.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akibadilishana mawazo na Mama Salma Kikwete walipowatembelea wagonjwa wa fistura (hawapo pichani) kwenye hospitali ya CCBRT.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mama Daniella Schadt wakitembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya CCBRT iliyoko huko Msasani Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na mgeni wake Mama Daniella Schadt, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani mara baada ya viongozi hao kutembelea hospitali ya CCBRT huko Msasani (PICHA NA JOHN  LUKUWI).

No comments: