Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa
jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi.Tanzania Girl
Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda
mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua
ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo. (wanne kulia ni
Naibu waziri wa Afya Dk.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Leonidas Gama, Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na
wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dk.Cyril Chami.
Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la
upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro
muda mfupi baada ya kulifungua. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk,Steven
Kebwe.
Jengo la NSSF la kitega uchumi Moshi
Rais Dk.Jakaya Kikwete,Waziri wa Kazi na
ajira Mh.Gaudensia Kabaka(watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk.Ramadhani
Dau (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama(wapili kushoto)
pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega
uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Rais Dk.Jakaya Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF Dk.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya
la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa
hafla ya ufunguzi.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akiagana na mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Dk.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la
kitega uchumi la NSSF mjini Moshi.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.(Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment