KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Tuesday, February 10, 2015

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 -15 , 2015 mjini Singida.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi jana Jumapili tarehe 08 Februari, 2015 katika kikao chake cha kawaida.  Pamoja na kujadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 na 15 mjini Singida, Kamati ilijadili na kuamua yafuatayo:-

1.   Zoezi la utoaji leseni kwa vilabu litaanza kabla ya msimu wa ligi 2015/16.  Vilabu vitatumiwa fomu za maombi mapema iwezekanavyo ili viweke nyumba zao sawa na kuleta maombi.  Leseni za vilabu (club licence) ni agizo la CAF na FIFA katika kuhakikisha vilabu vinaendeshwa kwa weredi.  Baadhi ya maeneo yanayoagaliwa katika utoaji wa leseni ni pamoja na kuwepo kwa Sekretarieti, miundo mbinu ya mazoezi na mashindano, hadhi za kisheria (legal status) mikataba ya ajira n.k.

2.   Kamati ya Utendaji imeazimia kufanyika kwa mashindano ya Taifa Cup kwa upande wa wanaume.  Sekretarieti ya TFF imetakiwa kufanya juhudi ili mashindao hayo yaweze kufanyika.

3.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetoa pongezi kwa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa juhudi zake za kukuza soka la vijana kupitia mradi wake wa kuanzisha shule ya soka (Academy) kwa ushirikiano na klabu ya Real Madrid ya Hispania.  Aidha Kamati ya Utendaji ya TFF imeipongeza Kampuni ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa juhudi zao za kuchangia maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu kwa ujumla ikiwa ni kupitia mpango wa kujenga shule ya soka (academy) uwezeshaji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 13 (U-13) yatakayofanyika mwezi April, 2015 mjini Mwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya soka na michezo kwa ujumla.

Kamati ya Utendaji imewaomba wadau wengine kufuata mifano hiyo na kuchangia maendeleo ya soka kwani kazi hii inategemeana ni kwa faida ya wadau mbali mbali.

4.   Kamati ya Utendaji ilipokea mabadiliko ya uwakilishi wa Chama cha Soka la Wanawake nchini (TWFA) yaliyotokana na kuondoka kwa Bi. Lina Kessy aliyekuwa Mwenyekiti wake.  Bi. Lina ameajiriwa kama Afisa michezo wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.  Nafasi ya Mwenyekiti inachukuliwa na Bi. Rose Kisiwa ambaye hapo kabla alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TWFA ataendelea kuwa Mwenyekiti mpaka hapo utakapokaa Mkutano Mkuu wa kawaida wa TWFA.

5.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo kwa vitendo vya vurugu na utovu wa nidhamu katika mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini.  TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu hususani viongozi wa vilabu kutilia mkazo elimu ya kujitambua ili wachezaji wajue kuwa wao ni hazina ya Taifa na kioo (taswira) cha jamii, hivyo waepuke vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.  Vitendo hivi si tu vinakwamisha maendeleo, bali pia vinawadharirisha wao, mpira wa miguu na jamii kwa ujumla.

Kufuatia matukio ya hivi karibuni na kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu kwa haraka na weredi, Kamati ya Utendaji imeteua ya Kamati ya kuangalia na kusimamia kanuni za uendeshaji Ligi. Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Bodi ya Ligi, Kurugenzi ya mashindano, Kamati ya mashindano na kamati ya waamuzi.

                                                                                              
TFF YATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA FIF
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la soka nchini Ivory  Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
Katika salam zake Bw. Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa huo wa Afrika kwa mara pili.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha mpira wa miguu nchnii Misri (EFA ),kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha  Zamalek na ENPPI.
Mashabiki wapatao ishirini na moja (22)  wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kupelekea Shirikisho la Soka nchini Misri kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.
Katika salam zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu  katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.

TFF YAIPONGEZA CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Bw Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Bw Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika nchini  Equatorial Guinea bila ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
Katika salamu hizo kwenda kwa Bw Haytou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Bw Hicham El Amrani, Bw Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: