Kamati ya
Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu
beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya kinidhamu
aliyoyafanya akiwa uwanjani.
Osei
ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa
Yanga, Amisi Tambwe ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa
kwa kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Mlalamikiwa
alifika mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam,
Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri
kwa kitendo hicho.
Akisoma
uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei
alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti
yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili ya
Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia Ibara ya 96(3) ya Kanuni ya Nidhamu ya TFF
Toleo la 2012.
Katika
uamuzi wake, Kamati imesema kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa
kiungwana (fair play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni
dhaifu, hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.
Katika
hatua nyingine Kamati hiyo, imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona,
na Katibu wa Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.
Kwa upande
wa Sorogo, Kamati imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa
upande mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi
ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.
Badala
yake aliyehusika ni Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua
hatua dhidi yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya
Kamati ya Nidhamu ya SIFA.
Pia barua
ya kumsimamisha kocha huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa
Mashindano. Kamati imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo
maana hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi
na yametupwa.
Kwa
upande wa Galibona ambaye ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa
alishiriki kuhamasisha marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) kati ya Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa
aliwasilisha vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.
Kamati
imesema licha ya ripoti ya Saleh Mang'ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya
refa huyo na msaidizi wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada
ya tukio hilo hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.
Pia barua
ya FAM kwenda TFF kuhusu matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa,
hivyo Kamati imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na
yametupiliwa mbali.
KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI
600,000/-
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa
Squad, Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao
haukufuata kanuni za usajili.
Villa
Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala
ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad
ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki
ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko
ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad
kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni
mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita
mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili
majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala
la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi
thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of
doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda
ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu
hiyo.
JKT
MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu
ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada
ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu
kwenye mechi.
Uamuzi
huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza
malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa
sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.
Kamati
imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi
yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo
ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale
imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia
malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi
yake ya mwisho ya ligi.
JUDICIAL AND
STANDING COMMITTEES.
Kamati
ya Utendaji iliyoketi tarehe 19 Disemba 2014, ilifanya mabadiliko katika kamati
ndogo ndogo na zile za kisheria. Kamati hizo ni kama ifuatavyo
KAMATI YA
NIDHAMU
1.
Tarimba Abbas (Mwenyekiti)
2.
Advocate Jerome Msemwa ( Makamu
mwenyekiti)
3.
Kassim Dau
4.
Nassoro Duduma
5.
Kitwana Manara
KAMATI YA
RUFANI YA NIDHAMU
1.
Advocate Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti)
2.
Advocate Revocatus Kuuli (Makamu
mwenyekiti)
3.
Abdala Mkumbura
4.
Dr. Franics Michael
5.
Advocate Twaha Mtengela
KAMATI YA
MAADILI
1.
Advocate Wilson Ogunde (Mwenyekiti)
2.
Advocate Juma Nassoro (Makamu mwenyekiti)
3.
Advocate Ebenezer Mshana
4.
Geroge Rupia
5.
Mh. Said Mtanda
KAMATI YA
RUFANI YA MAADILI
1.
Advocate Walter Chipeta (Mwenyekiti)
2.
Magistrate George Kisagenta (Makamu mwenyekiti)
3.
Lilian Kitomari
4.
Advocate Abdala Gonzi
KAMATI YA
UCHAGUZI
1.
Advocate Melchesedeck Lutema
2.
Advocate Adamu Mambi (Makamu
mwenyekiti)
3.
Hamidu Mahmoud Omar
4.
Jeremiah John Wambura
5.
John Jembele
KAMATI YA
RUFANI TA UCHAGUZI
1.
Advocate Julius Lugaziya (Mwneyekiti)
2.
Advocate Machare Suguta (Makamu
Mwenyekiti)
3.
Idrisa Nassor
4.
Paschal Kihanga
5.
Benister Lugora
KAMATI YA
FEDHA NA MIPANGO
1.
Wallace Karia (Mwenyekiti)
2.
Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti)
3.
Goodluck Moshi
4.
Omar Walii
5.
Ellie Mbise
6.
Deo Lubuva
KAMATI YA
MASHINDANO
1.
Geofrey Nyange (Mwenyekiti)
2.
Ahmed Mgoyi (Makamu mwenyekiti)
3.
James Mhagama
4.
Stewart Masima
5.
Steven Njowoka
6.
Said Mohamed
KAMATI YA
UFUNDI
1.
Kidao Wilfred (Mwenyekiti)
2.
Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti)
3.
Vedastus Rufano
4.
Dan Korosso
5.
Pelegriunius Rutahyugwa
KAMATI YA
MPIRA WA MIGUU YA VIJANA
1.
Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti)
2.
Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti)
3.
Ali Mayay
4.
Mulamu Ngh’ambi
5.
Said Tully
KAMATI YA
MPIRA WA MIGUU WANAWAKE
1.
Blassy Kiondo (Mwenyekiti)
2.
Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti)
3.
Zena Chande
4.
Amina Karuma
5.
Zafarani Damoder
6.
Beatrice Mgaya
7.
Sofia Tigalyoma
8.
Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati)
KAMATI YA WAAMUZI
1.
Saloum Umande Chama (Mwenyekiti)
2.
Nassoro Said (Makamu mwenyekiti)
3.
Charles Ndagala (Katibu)
4.
Kanali Issaro Chacha
5.
Soud Abdi
KAMATI YA
HABARI NA MASOKO
1.
Athuman Kambi (Mwenyekiti)
2.
Alms Kasongo (Makamu Mwenyekiti)
3.
Rose Mwakitangwe
4.
Amir Mhando
5.
Haroub Selemani
KAMATI YA
UKAGUZI WA FEDHA
1.
Ramdhan Nassib (Mwenyekiti)
2.
Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti)
3.
Jackson Songora
4.
Golden Sanga
5.
Francis Ndulane
6.
Cyprian Kwiyava
KAMATI YA TIBA
1.
Dr. Paul Marealle (Mwenyekiti)
2.
Dr. Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti)
3.
Dr. Mwanandi Mwankewa
4.
Dr. Eliezer Ndelema
5.
Asha Mecky Sadik
KAMATI YA
FUTSAL NA BEACH SOCCER
1.
Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2.
Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti)
3.
Samson Kaliro
4.
Shaffih Dauda
5.
Boniface Pawassa
6.
Apollo Kayugi
PRESIDENTIAL
COMMISSION FOR AFFAIRS
1.
Omar Abdulkadir (Mwenyekiti)
2.
Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti)
3.
Victor Mwandiki
4.
Riziki Majala
5.
Zahra Mohamed
6.
David Nyandu
PRESIDENTIAL
COMMISSION ON BUSINESS AND INVESTMENTS
1.
William Erio (Mwenyekiti)
2.
Mbaraka Igangula
3.
Advocate Iman Madega
4.
Lt. Col Charles Mbuge
5.
Philemon Ntalihaja
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment