KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, April 16, 2015

WAZIRI SAMUEL SITTA,ATANGAZA KUMUONDOA KABISA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) KAIMU MKURUGENZI MKUU MADENI KIPANNDE NA KUWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL)

Viongozi watano wa Kampuni ya reli Tanzania (TRL) wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa ununuzi wa Mabehewa Mabovu ya kubebea mizigo.
Uchunguzi umebaini kuwa
1.Mabehewa mengi kati ya yaliyoagizwa yana kasoro.
2.Kulikuwa na uzembe katika uagizaji na ufuatiliaji kiwandani yalipokuwa yanatengenezwa
3.Kulikuwa na uzembe katika kuendelea kuyapokea mabehewa hayo pamoja na ubovu wake kujulikana.
Hivyo Waziri mwenye dhamana ametangaza kuwasimamisha kazi viongozi wakuu wa TRL.
Viongozi hao ni;
1.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni,Kapallo Kisamfu
2.Mhandisi Mkuu wa Mitambo wa Kampuni,Ngosomwile Ngosomiles.
3.Mhasibu Mkuu wa Kampuni,Mbaraka Mchopa.
4.Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni,Jasper Kisiraga na 
5.Meneja Mkuu wa Manunuzi wa Kampuni,fedinarnd Soka.

Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta,(kushoto) akizungumza na waandishi Dar es Salaam kuhusu hatua alizochukua za kumuondoa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Madeni Kipande na kuwasimamisha kazi viongozi wakuu wa Kampuni ya reli Tanzania (TRL) kupisha uchunguzi wa ununuzi wa mabehewa mabovu ya kubeba mizigo.

No comments: