Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza
(aliyeinua mkono), akiuonyesha kidole ukuta wa nyumba ambao mmiliki wake
amegoma kuuvunja kupisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigambo, alipofanya ziara
ya kutembelea miradi ya Uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Dar es Salaam jana. Wengine (mwenye suti nyeupe ni Meneja Mradi
wa Ujenzi wa Daraja hilo, Mhandisi Karim Mataka na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa
NSSF, Juma Kintu (kulia).
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mataka, akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (kulia), kupita kwenye daraja la muda, alipotembelea miradi ya Uwekezaji inayofanywa na NSSF Dar es Salaam.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza
(katikati), akionyesha moja ya ramani za nyumba za kisasa zinazojengwa na
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika eneo la Kijichi, Kigamboni,
alipotembelea miradi ya uwekezaji inayofanywa na NSSF, Dar es Salaam jana.
Kulia ni Meneja Mradi wa shirika hilo, Mhandisi Karim Mataka na Mtendaji Mkuu
wa mradi wa Dege Eco, Mhandisi Julius Nyamuhokya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (mwenye suti nyeusi), akimsikiliza kwa makini Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mataka kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati akimweleza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment