Utangulizi;
-Marekebisho
ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom yamezingatia mechi za viporo za timu
za Azam na Yanga zinazoshiriki mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa
Afrika na Kombe la Shirikisho).
-Pia
ushiriki wa Azam na Yanga katika mechi zijazo za mtoano (play offs)
zinazokutanisha timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na
zile zilizosonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho.
-Iwapo
Azam itasonga mbele itacheza mechi hizo za mtoano, wakati Yanga yenyewe
itacheza tu mechi hizo za mtoano iwapo itatolewa katika raundi
inayofuata ya Ligi ya Mabingwa. Hivi sasa Azam na Yanga zinashiriki
hatua ya 16 bora ambayo itachezwa kati ya Aprili 8-10 kwa mechi za
nyumbani, na Aprili 19 na 20 kwa mechi za ugenini.
-Mechi
za kwanza za raundi ya mtoano (play offs) zitachezwa kati ya Mei 6-8
wakati za marudiano zitafanyika Mei 17-18. Yanga ikiitoa Al Ahly maana
yake haitacheza hatua ya mtoano (play offs), na badala yake itasubiri
moja kwa moja hatua ya makundi ambayo mechi zake za kwanza zitafanyika
kati ya Juni 17-19.
-Marekebisho mengine yanaweza kufanyika kwa kuzingatia matokeo ya scenario hizo hapo juu.
Wasalaam,
Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
No comments:
Post a Comment