Meja Jenerali January Kisanko, wakati wa uhai wake.
JESHI LA ULINZI LA
WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo
: “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku
la Posta 9203,
Telex
: 41051 DAR ESSALAAM, 22 Machi, 2016.
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe
: ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti
: www.tpdf.mil.tz
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina sikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali January Claudio Kisanko
(mstaafu) kilichotokea tarehe 21Machi 2016,
Meja Jenerali January Kisanko (mstaafu)
alizaliwa mwaka 1945 katika kijiji cha Mkima, Tarafa ya Lyangalile, Wilaya ya
Sumbawanga. Alipata Elimu ya Msingi Mkoani Rukwa na baadaye elimu ya Sekondari
katika Shule ya Sekondari ya wavulana Agakhan ambayo kwa sasa ni shule ya
Sekondari Tambaza, hadi alipohitimu kidato cha Sita mwaka 1966.
Marehemu Meja Jenerali January Claudio Kisanko
(Mstaafu) alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 31 Mei,
1967 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 24 Julai, 1969.Marehemu alilitumikia Jeshi
kwa muda wa miaka 35 na mwezi 1 hadi alipostaafu utumishi Jeshini
tarehe 30 Juni 2002.
Katika utumishi wake marehemu alishika Madaraka
mbalimbali Ikiwemo Kamanda wa patuni Nachingwea 1969 hadi 1970, Kamishina wa
Mipango na Sera katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa 2001, madaraka
ambayo alikuwa nayo hadi alipostaafu tarehe 30 Juni 2002.
Marehemu
Meja Jenerali January Kisanko (Mstaafu) alifariki dunia tarehe 21 Machi, 2016
katika Hospitali ya TMJ Dar es salaam. Ameacha Mke na Watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 28 Machi, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi
Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es
Salaam, saa 10:00 jioni.
MUNGU
AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA
JENERALI JANUARY KISANKO (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi,
Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano
zaidi: 0784-477638
No comments:
Post a Comment