Wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam wakimsikilza Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwahutubia wakati wa hafla ya kukabihi madawati yaliyotolewa na Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya
Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni,
Yusuph Mwenda akiwahutubia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya kupokea
madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya kusaidia
maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo, Yusuf Esack Ayub, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah (kushoto)
na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura (kulia).
Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat,Yusuf Esack Ayub akisaidiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kukata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 160 pamoja na vifaa mbalimbali kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa Shule hiyo, Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni wanachama wa taasisi hiyo, walimu na wanafunzi shule hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat, Yusuf Esack Ayub (kulia) akikabihi madawati 160 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndiyetabura kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Yusuph Mwenda, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah, Katibu wa taasisi hiyo, Ayub Esack (kushoto), waalimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya
Sekondari Mikocheni, Yusuph Mwenda (mwenye tai nyekundu) akizungumza jambo na
Afisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Sunza baada ya kupokea
Printer na madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya
kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo, jijini.
Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura.
No comments:
Post a Comment