Na
Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wa jumla
ya kiasi cha shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo lililokuwa
limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.
Kiasi
hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 15.43 ukilinganisha na makusanyo ya awali
ya mwaka 2015 ambapo mamlaka hiyo ilikusanya jumla ya kiasi cha shilingi
Bilioni 914.
Takwimu
hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard
Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jjijini Dar es Salaam.
“Kwa
mwezi Julai mwaka huu makusanyo yameongezeka kwa asilimia 15.43 ukilinganisha na
kipindi cha mwezi Julai 2015 ambapo tulikusanya shilingi Bilioni 914” alisema Kayombo.
Aidha
aliongeza kuwa mamlaka imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha kuwa inafikia au
inavuka lengo la Serikali la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa mwaka wa fedha
2016/2017 huku mkakati mmoja wapo ukiwa ni kuhakikisha kuwa walipa kodi wapya
wanasajiliwa zaidi.
Bw.
Kayombo aliongeza kuwa mkakati mwingine ni kuhuisha taarifa za walipa kodi kwa
kuhakikisha kwamba namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) zisizotumika
zinafutwa katika mfumo wa TRA.
Pia
amefafanua kuwa maandalizi ya kuhuisha taarifa za walipa kodi yapo katika hatua
za mwisho ikiwemo upigaji picha,uchukuaji wa alama za vidole pamoja na
vielelezo muhimu.
TRA
inawakumbusha wananchi kuhakikisha
wanakagua tiketi/ risiti zao za manunuzi na kuangalia usahihi wa pesa
walizolipa na uhalali wa risiti yenyewe.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo,akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana
kuhusu Makusanyo ya Kodi mwezi Julai mwaka huu kiasi cha shilingi Trilioni
1.055 sawa na asilimia 95.6.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo, (kulia) akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu Makusanyo ya Kodi mwezi Julai mwaka huu kiasi cha shilingi Trilioni 1.055 sawa na asilimia 95.6. Mwengine ni Meneja TRA Makao Makuu,Gabriel Mwangosi.
No comments:
Post a Comment