Na Beatrice
Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam.
SERIKALI imesema muswada
wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi
jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa
hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.
Akizungumza katika
mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari
kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe
maoni yao ili kuuboresha zaidi.
“Sifa moja ya taaluma
ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari
kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo
mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba
radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.
Kwa mujibu wa Abbas
alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa
waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na
kutoa ufafanuzi wa jambo husika.
Aidha Abbas alisema
kuwa ipo misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika mikataba ya kimataifa
ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki
ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo
suala la usalama wa taifa.
Aidha Abbas aliongeza
kuwa muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa wanahabari kwani unazungumzia
hali halisi ya mwandishi wa habari ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka
1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari pekee.
Mkurugenzi Abbas
alisema kila taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati kwa Tanzania
napo kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki taaluma ya habari.
No comments:
Post a Comment