Na
Beatrice Lyimo.MAELEZO
Dar
es Salaam
SERIKALI imeahidi
kuendeleza uhusiano na ushirikiano na vyombo vya habari nchini ili kuviwezesha
kutelekeleza vyema wajibu wake kwa umma.
Akizungumza katika
wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za Vyombo vya habari
leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari Hassan Abbas alisema lengo la
Serikali ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa chachu ya maendeleo ya
wananchi nchini.
Aliongeza kuwa yapo
mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Serikali katika sekta mbalimbali nchini
ikiwemo umeme, maji, barabara, afya, elimu, ambapo taarifa za utekelezaji wa
ahadi hizo za Serikali hazijaweza kuandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari.
Abbas alisema katika
kuimarisha mfumo wa utoaji wa habari na taarifa kwa umma, ofisi yake kwa
kushirikiana na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) wameanzisha kipindi cha TUNATEKELEZA ambacho kinatoa fursa kwa
Viongozi wa Serikali kutoa taarifa kwa umma kuhusu utelekezaji wa mipango
mbalimbali ya Serikali.
Aidha Abbasalisema
ofisi yake ndiye msimamizi na mratibu mkuu wa vitengo vya mawasiliano Serikali,
hivyo alitoa wito kwa wanahabari kuwasiliana naye mara kwa mara pindi
wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa taarifa katika
ofisi za umma.
Kuhusu mafunzo kwa
wanahabari, Abbas alivitaka vyombo vya habari kutumia fursa ya waandishi
wakongwe waliopo katika ofisi zao, ambao wamebobea katika maeneo mbalimbaloi
ikiwemo uandishi wa makala, habari na upigaji picha.
No comments:
Post a Comment