UONGOZI
wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu
wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu
na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.(kulia pichani chini)
Agosti
mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya
kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la
ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam
Complex.
Agyei anasaini
mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo
Kombe la Shirikisho Afrika.
Tunaamini
ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17,
utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni,
hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa kipindi chote atakachokuwa
akiipigania jezi ya Azam FC.
Azam FC
tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho
kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi
hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya
Kimataifa.
Lengo
kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata matokeo
bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi tulilokuwa nalo, wachezaji
wazuri walioko kikosini na wengine watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza
kutuvusha kuelekea safari ya mafanikio msimu huu.
Hivyo, tunawaomba
mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu kwani tunaamini ya
kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika kuwapa hamasa wachezaji ya
kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu kiujumla.
Wakati
huo huo, leo tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya kujiunga
na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil
Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),
Wengine
ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote
Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.
Imetolewa na Uongozi Azam FC
No comments:
Post a Comment