Viongozi wa Umoja huo na wanafunzi.
Wanafunzi.
Viongozi.
Viongozi.
Shule na wanafunzi.
TAARIFA
FUPI YA SHULE YA MSINGI GULUKA KWALALA
KWA WAGENI UVCCM MKOA WA DARA ES SALAAM TAREHE 16/11/2016
Ndugu kiongozi wa
msafara wa umoja wa vijana wa chama cha
Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es salaam
kwa niaba ya uongozi wa shule yaani kamati ya shule ukiongozwa na
mwenyekiti wetu Prof Felician Barongo, Walimu, Wanafunzi na wanajamii zima ya shule hii Guluka kwalala
tunapenda kuwakaribisha sana kwani ni mara ya kwanza kupata ugeni hapa shuleni wa
namna hii tangu shule hii imeanzishwa
miaka sita iliyopita.
Shule ya Msingi Guluka
kwalala iliyoanzishwa mwezi januari 2011
ikiwa na wanafunzi 250 na ikiwa na
darasa la I sasa hivi ina jumla ya wanafunzi wapatao 1326 kwa
mchanganuo ufuatao;-
Awali - 51
1 - 290
II - 189
III - 218
IV - 147
V - 221
VI - 210
JUMLA - 1326
Shule hii ina walimu
wapatao 17 wakiume 3 na wakike 14 ikiwa na usumbufu wa walimu 14 kutokana na
ikama inayotakiwa
Kwa upande wa kamati
shule yetu hakuna tatizo kwani ina wajumbe 13
kama waraka wa Elimu unavyoelekeza ambayo imechaguliwa June 2015 na itahudumu hadi 2019 June
Kwa upande wa vyumba
vya madarasa shule ina vyumba vya madarsa vitano (5) ikiwa inaupungufu wa vyumba 23 ukiunganishwsa na idadi ya wanafunzi,
shule haina ofisi ya walimu kwani walimu wanakaa madarasani na wanafunzi kitu
ambacho sio sawa kutokana na taratibu. Pia shule ina upungufu mkubwa wa matundu
ya vyoo kwani mahitaji ni matundu 58 lakini yaliyopo ni sita (6) tu
Kwa upande wa taaluma
shule yetu haiku vibaya kwani pamoja na shule hii kutokufika darasa la saba lakini kwa
darasa la IV kwa miaka waliyofanya
mitihani ya upimaji wa kitaifa haijafanya vibaya hata mara moja wanafunzi wote
waliokuwa wanafanya mitihani ya Taifa wamekuwa wanafaulu kwa 100% na hata mwaka huu matarajio yetu ni kufanya vizuri kwani matokeo ya kanda
ya Ukonga ambayo ina shule 64 kwa mtihani
wa Mock uliofanyika hivi karibuni imeshika nafasi ya 34 na kwa matokeo hayo yameifanya shule yetu
kushika nafasi ya 3 kati ya shule 7 za Kata ikizidiwa na shule za matajiri wawili yaani za
private Highmount na Rugwa na kuziacha shule 5 chini kwa kufaulisha wote
waliofanya mtihani huo. Nachukua nafasi
hii kuwapongeza walimu na kamati ya
shule kwa jitihada zao za kufanikisha matokeo haya japo walimu
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo msongamano wa wanafunzi
wengi madarasani, uhaba mkubwa sana wa vitabu vya kiada na mwamko mdogo wa wazazi kwani kwa kutojua wajibu wao kwa
watoto wao wamediliki kusema Elimu bure hivyo hawawezi kuchangia chochote hata
kununua vitabu kwa watoto wao. Wanategemea Serikali iwaletee. Kwa upande wa samani za shule kuna uhaba wa samani kama viti na meza kwa ajili ya walimu kwani tuna hitaji viti 30 na meza
17 lakini vilivyopo ni viti 8 na meza 5 tu.
TATIZO
LA VITABU VYA KIADA
Shule yetu inakabiriwa
wa uhaba mkubwa wa vitabu vya kiada kwa madarasa la V,VI na sasa VII kwani madarasa haya tangu yameanza hayajapata
vitabu toka serikalini kwa madarasa
ya V na VI ina vitabu visivyozidi
vitano kwa kila darasa hii ni kutokana na juhudi za
uongozi wa shule kupita kuomba nakala
moja moja kwa shule jirani na hivyo kuwafanya walimu kuwa na kopi mojamoja za kufundishia. Januari 2017 shule
yetu itakuwa na darasa la VII kwa mara ya kwanza lenye wanafunzi 210 na
kuhitaji vitabu vya kiada kwa masomo yote kumi (10) hatuna hata nakala ya kitabu kimoja.
Ni matumaini ya shule
yetu ziara yenu hii italeta tija kwa
walimu na wanafunzi wa shule kwa kuzingatia kuwa nyinyi ni watu mnaotoka katika
Chama chenye Serikali hivyo ni jukumu
lenu kumsaidia Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake
la kutoa Elimu bila malipo ambalo utekelezaji wake umeanza mwenzi Januari 2016.
Pia pamoja na kuomba
msaada wa vitabu tunaomba pia kusaidiwa miundo mbinu ya maji kwani shule haina
kisima cha maji, na shule haina nishati ya umeme. Mwisho tunaomba msaada wa
Uniform inayojulikana T-shirt ambazo huvaliwa jumatano kama leo na ijumaa
lakini haturuhusiwi kupokea fedha ya mzazi yeyote kwa ajili ya sare hii lakini
bado hakuna tamko lolote linalositisha uvaaji wa sare hizi
Tunayomengi lakini kwa
leo tunaomba niishie hapo kwa kuwa ninyi ni watu wazima kwa maelezo niliyoyatoa
mmeelewa na hivyo kufika mahali kuweza kusaidia shule iweze kupiga hatua ya
maendeleo kwani wazazi wa eneo hili wameathiriwa sana na siasa hivyo nao wako kama wanasiasa na
kusahau majukumu ya kusaidiana na walimu kuleta maendeleo ya shule na watoto wao.
Mwisho sisi wanajumuiya
ya shule tumefarijika sana na ujio wenu
hapa shuleni na kutia moyo kwa kuleta msaada huu mkubwa kwa wanafunzi wetu na
tunawaahidi msaada huu utaleta chachu ya maendeleo ya kitaaluma na kuinua
ufaulu wa shule yetu .
Karibuni tena siku nyingine
Ahsanteni sana
HAPA
KAZI TU
………………………..
Valentine
F. Mhagama
Mwalimu
Mkuu
No comments:
Post a Comment