KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Tuesday, November 22, 2016

MAHAFALI YA 9 YA CHUO CHA KODI KUFANYIKA DESEMBA 17, 2016.



MAHAFALI YA TISAYA CHUO CHA KODI
Chuo cha Kodi kinapenda kuwatangazia wahitimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 na Umma kwa ujumla kuwa Mahafali ya Tisa (9) yatafanyika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumamosi tarehe 17 Desemba, 2016, kuanzia saa Tatu asubuhi. Katika mahafali hayo wahitimu wa programu zifuatazo watatunukiwa astashahada, stashada na shahada:

1. Cheti Cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki(CFFPC)
2. Stashahada ya Usimamizi Wa Forodha na Kodi (DCTM)
3. Shahada Ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM
4. Astashahada ya Uzamili ya Uongozi wa Forodha ya Africa Mashariki (PGCCA)
5. Stashahada Ya Uzamili Katika Kodi (PGDT)

Wahitimu wote wanaopenda kushiriki wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

1. Kuthibitisha kabla ya tarehe 8/12/2016, kwa Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala kwa maandishi kuwa watashiriki.

2. Kulipia kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya joho na kuwasilisha stakabadhi ya malipo kwa Makamu Mkuu wa Chuo kabla ya 8/12/2016. Malipo yote yafanyike kupitia Benki ya CRDB, Akaunti ITA Fee Collection Account No. 0150303205600.

3. Wahitimu waliolipia watachukua majoho na kuhudhuria mazoezi Ukumbini siku ya Ijumaa tarehe 16/12/2016, saa 3.00 asubuhi.

Wahitimu watakaoshiriki watagharimia usafiri na malazi yao kwa kipindi chote watakapokuwa Dar es Salaam kwa ajili ya mahafali.

Tafadhali mjulishe na mwingine.

Wote mnakaribishwa

Imetolwana:
Mkuuwa Chuo,
ChuochaKodi
Eneo la Viwanda MIKOCHENI "B",
S. L. P. 9321, Dar es Salaam.
Simu: +255 22 2925100
Baruapepe:ita@tra.go.tz

No comments: