Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Mhandisi Decklan Mhaiki, akiwasilisha mambi ya shirika hilo ya kupaandishi bei ya umeme kwa asilimia 18.9 wakati wa kikao cha majadiliano baina ya wadau na uongozi wa shirika, kilichoitishwa na Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), na kufanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 23, 2016.
Baadhi ya viongozi wa TANESCO na wadau wakifuatilia mjadala
Na
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wadau wa umeme kujadili
maombi ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ya kupandisha bei ya umeme kwa
asilimia 18.9 kwa uwazi na bila hofu lakini wakizingatia nia ya Serikali ya
awamu ya tano ya kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda.
Akifungua
majadiliano ya wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zanzibar na uongozi wa TANESCO jijini Novemba 23, 2016
kwenye ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Maji na Nishati,
(EWURA), kuhusu mapendekezo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi,
(pichani juu), ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Paul Makodna alisema, “Rais wetu Mh. Dkt.
John Pombe Magufuli, amedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ambao utafanikiwa tu
endapo tutakuwa na umeme wa uhakika na ulio bora.” Alisema.
Aliwataka
wadau kusikiliza kwa makini hoja za TANESCO zinazowasukuma kupandisha bei ya
umeme, lakini TANESCO nao wanapaswa kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu
mapendekezo yao.
Akiwasilisha
mapendekezo ya TANESCO kwa wadau, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Decklan Mhaiki, alisema, Shirika hilo limefikia uamuzi wa kuwasilisha
mapendekezo hayo kulingana na mambo matatu ambayo ni kufua umeme (power generation),
Kusambaza umeme (Power distribution), na kusafirisha umeme (Power transmission).
“Kama
mjuavyo shirika limekuwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kuboresha
miundombinu ya umeme kote nchini, kwa lengo la kuwapatia wananchi umeme ulio
bora na wa uhakika, na kwakweli mabadiliko tayari yameanza kuonekana ambapo
hivi sasa kadri siku zinavyokwenda mbele hali ya umeme wetu imekuwa bora zaidi.”
Alsiema Mhandisi Mhaiki.
Alisema,
bei ya umeme hapa nchini ni ya chini ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika
Masharikiambapo alisema, wakati bei ya umeme kwa sasa, hapa Tanzania ni
shilingi 242.21, wakati Kenya bei ni Shilingi za Kitanzania, 326 kwa unit,
Uganda Shilingi 456 kwa unit, Rwanda Shilingi 438 kwa unit, na Burundi ni
Shilingi 195 kwa unit.
“
Hata tukipandisha umeme bado Tanzania bei ya umeme itabaki kuwa chini
ukilinganisha na majirani zetu ambapo, tunaomba unit moja ya umeme iuzwe kwa Shilingi
286.28, sawa na ongezeko la asilimia 18.9.” Alifafanua Mhandisi Mhaiki.
Akitoa
hotuba ya ukaribisho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), Felix Ngamlagosi, alisema, Mamlaka hiyo imepokea
maombi ya TANESCO kupandisha umeme kwa mwaka mmoja kuanzia Januari hadi Desemba
2017, kama ambavyo sheria inavyotaka.
“Mamombi
haya ya TANESCO ni halali yamekidhi sheria, na niwaombe wadau mtoe maoni ambayo
yatasaidia pande zote mbili, TANESCO na watumiaji wa umeme, ili hatimaye
wananchi waendelee kupata huduma bora ya umeme.” Alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema, tayari Mamlaka yake imekwisha kusanya maoni kutoka kanda
wakilishi zote nchini nab ado wanakaribisha maoni zaidi yatumwe kwenye mamlaka
yake hadi Novemba 25 mwaka huu saa 11 jioni ambapo dirisha la kupokea maoni
litafungwa.
Kwa
upande wa watoa maoni, Mwanasheria wa Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), Abas
Juma alsiema, kwa mujibu wa vigezo vilivyopelekea TANESCO kuomba bei ya umeme
ipande, ni viwili tu ndio vinaihusu ZECO, ambavyo ni uzalishaji na usafirishaji
umeme, na kwamba kazi ya kusambaza umeme inafanywa na ZECO yenyewe na kuliomba
shirika la umeme TANESCO kuzingatia uhalisia huo na hivyo ZECO haistahili
kulipa bei sawa nay a wateja wa TANESCO Tanzania bara.
Mwananchi
mwingine ambaye ni mzalishaji umeme kwa kutumia bio-gas, ameipongeza TANESCO
kwa kuboresha huduma zake na kuwataka wadau kulikubali ombi la Shirika hilo ili
kuwezesha kasi ya uboreshaji huduma iweze kusonga mbele.
“Mimi
ninaunga mkono maombi ya TANESCO, sisi wazalishaji umeme wadogo, tunashindwa
kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ya kuendesha miradi yetu maana mabenki
hayana uhakika kama tunaweza kurejesha fedha zao kwa vile bei ndogo ya umeme
inayotozwa na TANESCO hailingani na gharama za uendeshaji, hivyo wanahofia
wasiweze kupata fedha zao.” Alisema.
Mwananchi
mwingine ambaye ni Mfugaji aliipongeza TANESCO kwa kuboresha huduma za umeme na
sasa hali ya umeme imeanza kuimarika. “Mimi ni mfugaji miaka miwili iliyopita
nililazimika kununua taa za mchina, ili kuhudumia kuku wangu kwa vile umeme wa
TANESCO ulikuwa hautabiriki, lakini hivi sasa zile taa sio muhimu tena kwangu
kwani umeme unapatikana kwa uhakika lakini sio hivyo tu hata ubora wa umeme
wenyewe umekuwa wa kuridhisha sana.” Alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), Felix Ngamlagosi
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya EWURA
Baadhi ya wadau na viongozi wa TANESCO
Baadhi ya wadau kutoka Zanzibar na viongozi wa EWURA
Mkuu wa Wilaya Hapi, (kushoto) na Ngamlagosi, wakifurahia jambo
Mdau akitoa maoni yake
Mdau kutoka ZECO, Abas Jumaa, akitoa maoni ya ZECO
Wadau kutoka Zanzibar
No comments:
Post a Comment