Kocha Mkuu wa Timu
ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo
Novemba 04, 2016 ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho
kitasafiri wiki ijayo kwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo
wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mkwasa maarufu
kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Novemba 07,
2016 kabla ya kuanza kukiandaa kikosi hicho siku inayofuata ikiwa mara baada ya
michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako itakuwa funga
dimba la duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
LIGI
KUU YA VODACOM TANZANIA BARA RAUNDI YA 15
Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu
huu, inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja
sita.
Kwa
keshotwa Jumapili, African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo Na. 144 wakati Mbao itakuwa mwenyeji wa Azam
FC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
MAZUNGUMZO
YOUNG AFRICANS, SIMBA YAENDELEA VEMA
Mazungumzo
kati ya Viongozi wa Young Africans na Simba, katika shauri la madai,
yanaendelea vema na mwishoni mwa wiki hii huenda wakakamilisha kwa kuridhiana.
Viongozi
hao wamefanya hivyo kwa dhana kuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) inayosisitiza uungwana katika soka ikisema: “My Game is Fair Play”. Kwa upande
wa Young Africans, uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit wakati
upande wa Simba alikuwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
TWIGA
STARS KUIPIMA UBAVU CAMEROON
Waandaaji wa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016, wameipa heshima
Tanzania na kuona kuwa Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake inafaa kuipima
ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
Twiga
Stars ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya
taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya
kuwa kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini
zaidi ni mabinga wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu
huko Uganda.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/658-
Nyota wa Stars
walioitwa na Mkwasa ni:
Makipa
Deogratius
Munishi –Young Africans
Said Kipao –JKT Ruvu
Aishi Manula –Azam FC
Mabeki
Erasto Nyoni -Azam FC
Michael Aidan -JKT Ruvu
Mwinyi Haji -Young Africans
Mohamed
Hussein –Simba SC
David Mwantika -Azam FC
James Josephat –Tanzania Prisons
Vicent Andrew -Young Africans
Viungo
wa Kati
Himid Mao -Azam FC
Mohammed
Ibrahim –Simba SC
Jonas Mkude –Simba SC
Muzamiru
Yassin –Simba SC
Viungo
wa Pembeni
Abdulrahman
Mussa -Ruvu Shooting
Shiza Kichuy –Simba SC
Simon Msuva -Young Africans
Jamal Mnyate –Simba
Washambuliaji
Ibrahim Ajib –Simba
SC
John Bocco -Azam
FC
Mbwana Samatta -K.R.C
Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli –Oman
Thomas
Ulimwengu –Mchezaji huru
Omar Mponda -Ndanda
Kwa sababu
mbalimbali hususani majeruhi, Mkwasa amewaacha wachezaji Shomari Kapombe (Azam
FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Juma Abdul na Juma Mahadhi wa Young Africans.
Mchezo huo wa
kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa
kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na
kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni
mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo, nasi
mara moja tukakubali.
Hii ni faida
kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama
inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo
huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa
sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA
zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina
inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa
wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya
Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la
Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa
na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45).
Wachezaji wa
Zimbabwe watakaochuana na Tanzania ni makipa: Tatenda Mukuruva (Dynamos) na Donovan
Bernard (How Mine).
Mabeki:
Godknows Murwira (Dynamos), Hardlife Zvirekwi (CAPS United), Ronald Pfumbidzai
(CAPS United), Honest Moyo (Highlanders), Lawrence Mhlanga (Chicken Inn) na Teenage
Hadebe (Chicken Inn).
Viungo: Tendai
Ndlovu (Highlanders), Farai Madhanhanga (Harare City), Jameson Mukombwe
(Chapungu), Tafadzwa Kutinyu (Chicken Inn), Ronald Chitiyo (Harare City),
Talent Chawapihwa (ZPC Kariba) na Malvern Gaki (Triangle).
Washambuliaji:
Pritchard Mpelele (Hwange), Gift Mbweti (Hwange), Leonard Tsipa (CAPS United),
Rodreck Mutuma (Dynamos) na William Manondo (Harare City)
LIGI
KUU YA VODACOM TANZANIA BARA RAUNDI YA 15
Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu
huu, inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja
sita.
Kwa keshotwa Jumapili,
African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
katika mchezo Na. 144 wakati Mbao itakuwa mwenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.
Kwa upande
wake, Ndanda siku ya Jumapili itakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwenye mchezo Na 117 wakati
Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya katika mchezo Na. 118.
Kagera Sugar
kwa upande wake siku hiyo ya Jumapili itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba, mjini Kagera katika mchezo ulipewa Na. 119 ilihali JKT
Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko
Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo Na. 120.
Ligi hiyo
itaendelea Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City
kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro katika mchezo Na. 113 wakati Mwadui
itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga
katika mchezo ulipewa Na. 115.
MAZUNGUMZO
YOUNG AFRICANS, SIMBA YAENDELEA VEMA
Mazungumzo
kati ya Viongozi wa Young Africans na Simba, katika shauri la madai,
yanaendelea vema na mwishoni mwa wiki hii huenda wakakamilisha kwa kuridhiana.
Viongozi hao
wamefanya hivyo kwa dhana kuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) inayosisitiza uungwana katika soka ikisema: “My Game is Fair Play”. Kwa upande
wa Young Africans, uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit wakati
upande wa Simba alikuwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Katika kikao
hicho ambacho Msuluhishi wake, Wakili na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo
Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Said El – Maamry hakuhudhuria kwa
sababu za udhuru, Baraka wa Young Africans aliongozana na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa Young Africans, Omar Said pamoja na Mawakili Oscar Magolosa na Alx
Mushumbusi.
Kwa hali
halisi ya uchumi kwa sasa, timu hizo zimezungumza hadi kufikia mwafaka wa
kiwango kisichozidi Sh milioni 200 kutoka dola dola 600,000 (zaidi ya Sh
milioni 1,200 au Bilioni 1.2). Mazungumzo ya wikiendi hii yanakwenda
kukamilisha mvutano wao, kama ambavyo walikubaliana kwenye kikao kilichoketi
jana Novemba 03, 2016.
Madai makuu ya
Simba ni dhidi ya mchezaji Hassan Hamis Ramadhani maarufu kwa jina la Hassan
Kessy na dhidi ya Young kudaiwa kuvunja mkataba na kuingilia makubaliano mapya
wakati tayari mchezaji alikuwa na mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa
wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
TWIGA
STARS KUIPIMA UBAVU CAMEROON
Waandaaji wa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016, wameipa heshima
Tanzania na kuona kuwa Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake inafaa kuipima
ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
Twiga Stars
ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya
Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya kuwa
kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni
mabinga wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko
Uganda.
Rekodi hizo
zimesukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT)
– nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo kuomba
kucheza nayo mwishoni mwa wiki ijayo. Tayari Twiga Stars imeanza maandalizi ya
kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake Edna Lema na El Uterry
Mollel.
Kutokana na
kuitikia wito huo kutakuwa na mabadiliko kidogo ya ratiba kwa Ligi Kuu ya
Waanawake. Ligi hii itaendelea kama ilivyo kwenye ratiba kwa makundi yote
mawili ya A na B, isipokuwa kwa michezo miwili tu ambayo yote ni ya Kundi A.
Mchezo kati ya
JKT Queens na Viva FC kadhalika Evergreen Queens na Mlanduzi Queens, ambayo
itapangiwa tarehe nyingine. Michezo yote hii ilikuwa ichezwe tarehe 09.11.2016
kwenye viwanja vya Karume na Uhuru, Dar es Salaam.
Timu za JKT
Queens na Mlandizi Queens zina wachezaji zaidi ya wawili kwenye Twiga Stars
ambako JKT Queens wana wachezaji 11 na Mlandizi Queens ina wachezaji watatu.
..………………………………………………………………………… …………………..
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment