Na Beatrice Lyimo - MAELEZO
Mnamo Novemba Tano mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atatimiza mwaka mmoja tangu alipoapishwa kuongoza Nchi hii katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika uongozi wake wa mwaka mmoja, Sekta ya Utalii nchini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika kuongeza mapato ya serikali kupitia mikakati mbalimbali ambayo imeifanya kuwa sekta kuwa yenye manufaa zaidi ya kiuchumi.
Hatua hii inatokana takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinaoonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 idadi ya watalii waliongia nchini ilikuwa 1,376,182 na kuingizia mapato kiasi cha Dola za Marekani 1.9 bilioni.
Aidha
,idadi ya watalii walioingia nchini katika kipindi cha Julai mpaka Agosti
imeongezeka asilimia 11, na hivyo kuifanya ni eneo linaloiingizia Serikali
takribani asilimia 25 ya fedha za kigeni.
Kwa mujibu wa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Profesa Jumanne Mghembe anasema kwa
kuzingatia dhamira ya Serikali ya kujitegemea kiuchumi Wizara yake imeanzisha kodi ya
ongezeko la thamani (VAT) katika sekta ya utalii, hatua iliyolenga kuiongezea
Serikali mapato yatakayoweza kuchangia katika kutoa huduma za jamii.
“Uanzishaji
wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika sekta ya utalii, kumesaidia
kuongeza watalii nchini na mapato yamekuwa kwa asilimia 22 zaidi,” anasema
Waziri Maghembe.
Waziri Maghembe anasema uanzishaji wa VAT haujaathiri ongezeko la idadi
ya watalii nchini, na badala yake Tanzania inaendelea kuwa kimbilio la watalii
duniani
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa
na Wizara
ya Maliasili na Utalii, idadi ya watalii wanaoingia katika Hifadhi za
Taifa (TANAPA) katika kipindi cha Juni-Julai 2016 imeongezeka kwa wastani wa
asilimia 2.2 na mapato yatokananyo na viingilio hifadhini yameongezeka kwa
wastani wa asilimia 19.7
Huduma za malazi pia
zimekuwa zikitozwa kodi na Serikali hivyo kuondoa msamaha wa miaka 10
uliokuwepo awali na sasa vinachangia zaidi katika mapato ya nchi moja kwa moja
kwa kuondoa msamaha huo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na huduma
za utalii zimeanza kutozwa VAT kwa asilimia 18, lakini safari kwa ujumla
zimeongezeka kwa asilimia chini ya hiyo kwa sababu huduma za malazi zimekuwa
zikitozwa kodi hiyo tangu miaka ya nyuma.
Katika hatua hiyo Watalii mbalimbali waliohojiwa
nchini wameonyesha kuunga mkono hatua hiyo ya Serikali za kuwatoza kodi kwani fedha
zitakazokuwa zikilipwa na wataliii zitasaidia katika shughuli nyingine za
uchumi.
Pia katika kuendeleza
kutangaza Sekta ya Utalii nchini, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imetenga
kiasi cha Tsh Milioni 648 kwa ajili ya shughuli za utangazaji wa Utalii nje ya
nchi na Tsh.Milioni 300 kwa ajili ya utangazaji wa vivutio vya utalii wa ndani
ya nchi.
Wizara
ya Maliasili na Utalii inaendelea kutekeleza majukumu yake licha ya mabadiliko
na changamoto mbalimbali na inatarajiwa kuwa rasilimali za maliasili, malikale
na utalii zitaendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa juhudi za kukuza uchumi wa
Taifa.
Kwa
upande wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kipindi cha mwaka mmoja imeimarisha
utangazaji wa vivutio vya utalii kupitia mtandao wa kompyuta yaani Tourism
Destination Portal pamoja na mitandao ya kijamii kwa kuweka taarifa zaidi
za vivutio vya utalii katika tovuti hiyo maalumu ya utalii zikiwemo ramani
(digital map), picha za video na picha za mgando kwa kila kivutio cha utalii
katika tovuti hiyo.
Aidha,
TTB imeendelea kushirikiana na watu maarufu katika kutangaza utalii wetu.
Miongoni mwa watu hao ni wasanii wa ndani wakiwemo mchezaji maarufu wa Tanzania
anayecheza mpira wa miguu nchini Ubelgiji Mbwana Samatta na mwanamuziki Vanessa
Mdee.
Mpaka kufikia mwezi
Juni 2016 idadi ya watalii wa Kimataifa waliongia nchini ilikuwa ni 519,582
ikilinganishwa na watalii 504,711
waliongia nchini mpaka kufikia mwezi
Juni 2015.
Idadi hii ni sawa na
ongezeko la asilimia 2.86. Kwa kipindi cha miezi ya Julai na Agosti 2016
inaonyesha kuwa idadi ya watalii waliongia kwenye hifadhi za Taifa imeongezeka
kwa wastani wa asilimia 11.16.
Akiongea wakati wa
uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Magufuli
aliwataka mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje kutumia fursa zilizopo
katika kutangaza utalii wa nchi ili kuweza kuongeza pato la Taifa.
No comments:
Post a Comment