Shirikisho
la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limemteua Jonesia Rukyaaa -
Mwamuzi wa soka kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi wa kati 10
watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka huu.
Kwa
uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
amempigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa
ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za
kimataifa.
No comments:
Post a Comment