Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam.
SERIKALI imepanga
kununua ndege za kisasa ili kuimarisha ulinzi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Hayo yamesemwa jana na
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati
akihojiwa na kipindi maalumu cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha
Televisheni ya Taifa (TBC1).
Meja Jenerali Milanzi
anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika kulinda hifadhi zilizopo na ili kuweza
kukabiliana na ujangili unaojitokeza katika hifadhi mbalimbali nchini.
“Sekta ya Utalii
nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 na kutoa ajira kwa
zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali ya utalii nchini, hivyo
ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika kulinda vyanzo vilivyopo” alisema
Meja Milanzi.
Aidha, alisema kuwa
Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote
watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya magogo ili kulinda
hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.
Aidha Meja Jenerali Milanzi
aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda
misitu iliyopo kwa kutunza mazingira na hifadhi za taifa.
Mbali na hayo Meja
Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazovutia watalii
wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na
kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa ili kuzudi kuvutia watalii nchini.
No comments:
Post a Comment