Mamlaka
ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha watanzania tamaduni ,mila na desturi ili kuulinda utamaduni wetu , ambao unaonekana
kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza
na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo
hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali
za kitanzania .
Amesema
utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja
na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda
utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema
chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Communinity College cha
nchini Canada kinaanda kozi hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa
undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia
ya makabila mbalimbali.
Ayo
amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba
kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza
kutolewa.
Aidha
mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa
mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa
mitaala.
Ayo
amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika
kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza
kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa
rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro kuchangamkia
fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa sehemu ya wataalam watakaohudumia
viwanda vitakavyojengwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John
Pombe Magufuli kuweka msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda.
Caps 1.Mwalimu wa Ufundi
Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari
juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
Caps 2.Wanafunzi
wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiwa katika mafunzo ya vitendo
katika Chuo cha Mikumi
Caps 3.Mwalimu wa uChuo
cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari
walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Caps 4.Mwanafunzi wa
mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunnzo ya vitendo karakana
ya ufundi wa Magari.
caps 5.Sehemu ya maktaba ya
Chuo cha VETA Mikumi
No comments:
Post a Comment