Na
Ally Daud
MAELEZO
Dar
es Salaam
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la
kitaifa la Afya litakalofanyika Novemba 14 mwaka huu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Dkt. Omary Chillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
leo jijini Dar es salaam wenye lengo la kujadili maendeleo ya sekta afya nchini.
Aidha Dkt. Chillo alisema
kuwa kongamano hilo litajadili jitihada ilizofikia Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya
maendeleo ya kimkakati ya maisha yenye afya njema (SDG-3) yaliyokusudiwa kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya wachapakazi.
Dkt. Chillo aliongeza
kuwa kongamano hilo pia linatarajia kujadili mikakati ya kuboresha sheria ya
usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi nchini kwa ajili ya maendeleo ya wafanyakazi na usalama
wao.
Kwa mujibu wa Dkt. Chillo
alisema kuwa kongamano hilo pia linatarajiwa kufanyika kuwakutanisha wataalam
wa sekta ya afya 700 na kuratibiwa na taasisi tano zikiwemo MoHCDGEC,
TMHS,APHFTA,CSSC na BAKWATA.
Mkutano huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya,
zinatarajia pia kushiriki katika
maonesho ya bidhaa zinafanyika kwa
ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.
No comments:
Post a Comment