Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kunashukuru wanafamilia wa soka kwa
salamu mbalimbali za rambirambi kutokana na msiba wa Mwenyekiti wa Azam
FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad
aliyefariki dunia Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es
Salaam.
Hayati
Sheikh Said Muhammad kualikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo
katika Kamati ya Utendaji ya TFF.
Itakumbukwa
kwamba Sheikh Muhammad aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa
ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara
ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.
Kutokana
na kufariki kwa Sheikh Muhammed, Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amempendekeza Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Bwana Yahya Hamad - kukaimu
nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji Ligi (Kamati ya Saa 72) ili kushughulia masuala yote ya mechi zilizochezwa tangu mwanzo wa Novemba, 2016 baada ya kifo cha Sheikh Muhammad.
Tunachukua
nafasi hii kutoa wito kwa klabu kumpa ushirikiano Bwana Hamad katika
majukumu yake mapya akiongoza kamati hiyo yenye wajumbe ambao ni Baruan
Muhuza (Azam Tv), Boniface Wambura (Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi), Jonas
Kiwia (Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano TFF), Philemon Ntahilaja (Mdau wa
Mpira wa Miguu), Charles Ndagala (Katibu Kamati ya Waamuzi ya TFF),
Kanali Mstaafu wa JWTZ, Isaron Chacha na Steven Mnguto ambaye ni Mjumbe
wa Bodi ya ligi.
KUMEKUCHA AZAM SPORTS FEDERATION CUP
Azam
Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu,
itaanza rasmi kesho Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika
mkoani Tanga kwa kuzikutanisha Bingwa wa Mkoa wa Tanga, Muheza United na
Sifa Politan ya Temeke, Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini humo.
Siku
hiyo kabla ya mchezo kutakuwa na shamrashamra kupamba michuano hiyo
ambako wachezaji wa zamani wa Coastal Union na African Sports za Tanga
zitachuana kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa uzinduzi. Timu hizo za
maveterani, zitachezwa kuanzia saa 8.00 mchana.
Pia
kutakuwa na shamrashamra za wasanii walioandaliwa na Wadhamini Azam Tv
ambayo kwa msimu wa 2016/17 zimeongezwa timu 22 kutoka mabingwa wa
mikoa-- Muheza na Sifa Politan ni miongoni mwa timu hizo. Ongezeko hilo
tofauti na msimu uliopita ambako kulikuwa na timu 64.
Mwaka
huu kuna timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu zote
24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL)
na timu 22 za mabingwa wa mikoa. Mashindano hayo yatakuwa ni ya mtoani
na yataendeshwa kwa raundi tisa (9).
Raundi
ya Kwanza itashirikisha timu zote 22 za Mabingwa wa Mikoa katika
makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu
zitaingia raundi ya pili.
Raundi
ya Pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya
kwanza na kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya
timu zote kuwa 32 kwa hatua ya pili.
Raundi ya Tatu itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane zitakazoingia hatua ya nne.
Raundi
ya Nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha
timu nane (8) zilizoshinda Raundi ya Tatu (3) kufanya timu zote kuwa 32.
Raundi
ya Tano, itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya Nne (4) na kumuisha
timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya
timu zote katika raundi hii kuwa 32.
Raundi ya Sita itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika Raundi ya Tano na mzunguko huo utaitwa Hatua ya 16 Bora.
Raundi
ya Saba (7) itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na
mzunguko huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .
Raundi
ya Nane ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu Raundi ya Saba (Robo
Fainali) na mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni Nusu Fainali.
Raundi
ya Tisa itashirikisha timu mbili zilizofuzu Raundi ya Nane na washindi
hao wa Nusu Fainali na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa
msimu wa 2016/2017.
………………..………………………………………………………… ………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment