NCHI
inakwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam mbalimbali
katika kuweza kufikia uchumi huo kwa kuhitaji wataalam wanaozalishwa
nchini wakiwemo wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa na vyuo vya VETA.
Hayo ameyasema leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali
ya 46 katika Chuo cha VETA, Changombe Dar es Salaam,
amesema VETA inazalisha wataalam ambao wamebobea kwa ujuzi.
Amesema wahitimu wa VETA hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi
wanaoupata unawawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na
wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo walioajiriwa na kujiajiri.
Sabuni amesema wanaosoma VETA wapo waliohitimu kidato nne
hadi waliopata shahada ya kwanza hivyo
jamii iondoe dhana ya kwamba wanaosoma
VETA ni wale walioshindwa kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.
Aidha amewataka wahitimu wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na weledi katika kufanya kazi na kuondokana
kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi yao kupoteza sifa ya kujiajiri au
kuajiliwa.
Nae Mkuu wa Chuo cha VETA Changombe,
Douglas Kipokola amesema kuwa wahitimu mwaka huu wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo
tayari katika soko la ajira kutokana na mafunzo walioyapata.
Amesema kuna changamoto za walimu ambapo wameshaanza
kulifanyia kazi kutokana na mitaala inahitaji mafunzo yenye tija kwa uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi wasiozidi 20.
Mkuu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe Dar es Salaam, Douglas Kipokola akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo hicho.
Wahitimu wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe.
Sehemu ya wazazi katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe.
Wahitimu wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe.
Sehemu ya wazazi katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA , Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa
mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe.
No comments:
Post a Comment