KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, April 1, 2017

JE WEWE NI MIONGONI MWA WANAOSUBIRIA MWEZI APRILI KWA HAMU?.

JE WEWE NI MIONGONI MWA WANAOSUBIRIA MWEZI APRILI KWA HAMU?

Na Jumia Travel Tanzania.

Kama kuna kitu ambacho wafanyakazi wengi wanapenda kusikia basi ni sikukuu au mapumziko. Kwani hupata fursa ya kutokwenda kazini, haimaanishi kwamba ni wavivu bali kutokana na ufinyu wa likizo ukiachana na wikendi.

Kwa upande wa watanzania hali hiyo hutokea kwa baadhi ya miezi na wa Aprili ni mmojawapo. Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Jumia Travel, zifuatazo ni sababu zinazoufanya mwezi huu kupendwa zaidi nchini.


Sikukuu ya Karume. Hii siku huadhimishwa kila ifikikapo April 7 ya kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa visiwa vya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1972 katika eneo la Mji Mkongwe, Unguja. 


Hivyo basi kama taifa huiadhimisha siku hiyo kwa wananchi kupumzika na kutofanya shughuli yoyote na badala yake kumkumbuka shujaa huyo aliyeongoza mapinduzi dhidi ya waarabu waliokuwa wakivikalia visiwa hivyo kwa mabavu. Kwa mwaka huu ni tofauti kidogo kwani siku hiyo itaangukia Ijumaa na hivyo kutoa fursa kwa watu kupumzika kwa siku tatu ukijumuisha na wikendi. Kwa wenye mipango mifupi kwenye mapumziko hayo wanaweza kutekeleza azma zao, kama vile kusafiri nje kidogo ya mji. 

Sikukuu ya Pasaka. Kwa wakristo wengi nchini Tanzania na duniani kote kwa sasa wapo kwenye mfungo wa Kwaresma ambao ulianza tarehe mosi ya mwezi Machi na kudumu kwa siku 40. Kwa mujibu wa kalenda mfungo huo utaisha siku ya Alhamisi ya tarehe 13 ya mwezi Aprili. Maandalizi ya sikukuu ya Pasaka huanza siku ya Ijumaa Kuu, tarehe 14, ambayo ni siku ya mapumziko huku sikukuu yenyewe ya Pasaka itakuwa ni Jumapili ya tarehe 16. Lakini haiishii hapo kwani shamrashamra za Pasaka zitaendelea mpaka siku ya Jumatatu ya tarehe 17. Hivyo, kwa haraka haraka watu watakuwa na mapumziko ya siku nne mfululizo na ndio maana husubiriwa kwa hamu kubwa huku kukiwa na mipango lukuki ndani yake. 


Tembelea Jumia Travel kujua sehemu zilizo karibu nawe ambazo unaweza kwenda na kufurahia kwa siku hizo chache pamoja na wapendwa wako.

Sikukuu ya Muungano. Ifikapo tarehe 26 ya mwezi wa Aprili pia watanzania watakuwa na sherehe nyingine muhimu katika historia ya taifa lao. Siku hiyo inakumbukwa kwa Tanganyika kuungana na visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba) mnamo mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo ada siku hii nayo ni mapumziko kwa watanzania wote, watu hawaendi kazini na badala yake kusherehekea siku hiyo kwa kuutafakari umuhimu wa Muunganao na faida zake kwa wananchi wa pande zote mbili kwa pamoja.



Lakini mbali na sikukuu hizo pia kuna matukio kadhaa ambayo hunogesha mwezi huu kama vile:

Sikukuu ya wajinga. Hii ni siku ambayo husherehekewa kila ifikapo Aprili mosi ya kila mwaka ambapo watu na taasisi mbalimbali hufanya mizaha ya hapa na pale isiyo na madhara. Japokuwa siku hii ni maarufu miongoni mwa watu wengi duniani lakini hakuna taifa limeifanya kuwa ni siku ya mapumziko. Kwa nchi nyingi ikiwemo Tanzania, mwisho wa mizaha ambayo hufanywa siku hii huishia saa 4 asubuhi. Huazimishwa kwa kuunda utani na mizaha na watu watakaoiamini mizaha hiyo huitwa wajinga. Hivyo basi kuwa makini na siku hii ili usije ukapaziwa sauti ya “Sikukuu ya Wajinga!”

Nyama Choma Festival 2017. Kwa upande wa wapenda burudani nchini Tanzania mwezi wa Aprili kwao umo kwenye akili zao kwani lile tamasha kubwa ambalo huwakutanisha wapenda kula nyama wote jijini Dar es Salaam litafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 29. Tamasha hili huwaleta pamoja wachoma nyama mbalimbali pamoja na walaji kutoka kila kona ya jiji huku kukiwa na burudani kadhaa za muziki, vinywaji na shughuli nyinginezo. 



Tukio hili huvutia hadhira kubwa kadiri muda unavyokwenda kutokana na upekee wake na hivyo kupelekea kuwa maarufu na kusambaa mikoa mingine nchini.

Kwa hiyo kama ulikuwa hujui huo ndio mwezi wa Aprili ambao kwa watu wachache wamekwishasuka mipango yao tayari. Hujachelewa sana kwani kupitia Jumia Travel unaweza kupanga safari fupi karibu na eneo unaloishi ukaenda na kuwahi kurudi kuendelea na shughuli nyingine za kujenga taifa.

No comments: