Hivi
sasa majira ya saa moja usiku - Julai 10, mwaka huu kikosi cha timu ya
mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinasafiri kwenda jijini
Mwanza kwa Ndege ya Fast Jet ikiwa na ongezeko la wachezaji wapya saba.
Kati
ya hao ambao Kocha Mkuu Salum Mayanga amewaita, wamo wale
aliowatangaza juma lililopita ambao ni John Bocco, Kevin Sabato pamoja
na kinda Athanas Mdamu ambaye anacheza Alliance ya Mwanza inayoshiriki
Ligi Daraja la Kwanza.
Katika
kikosi chake kabla ya kuivaa Rwanda Jumamosi ijayo, wachezaji wengine
ambao Kocha Mayanga amewatangaza leo ni pamoja na Kipa wa Serengeti Boys
- timu ya taifa a vijana ya Tanzania, Ramadhan Kabwili.
Mbali
ya hao wamo pia Boniface Maganga kutoka Mbao FC, Joseph Mahundi kutoka
Azam FC na pia amemrejesha tena Said Ndemla wa Simba SC ambaye awali
alikuwa kwenye uangalizi wa majeraha.
Kikosi
hicho kinakwenda kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Jumamosi ya Julai 15, mwaka huu
Kipa
Benno Kakolanya, Shaban Idd Chilunda na Mbaraka Yussuf hao
wamepumzishwa kwa sababu ya majeraha waliyoyapata kwa nyakati tofauti
wakiwa na Taifa Stars huko Afrika Kusini kwenye michuano ya Kombe la
Castle la Cosafa - inayoandaliwa na Baraza la Soka kwa nchi za Kusini
mwa Afrika.
Pia wachezaji wa kimataifa ambao hawahusiki na mechi za CHAN ambao ni Thomas Ulimwengu na Elius Maguri, hawakuongozana na timu.
Timu
hiyo ilishika nafasi ya tatu katika michuano ya Castle Cosafa kwa
kuishinda Lesotho kwa mapigo 4-2 ya penalti katika mchezo uliofanyika
Uwanja wa Moruleng nchini Afrika Kusini Ijumaa iliyopita.
Mwanza
inajiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda unaotarajiwa kufanyika Jumamosi
Julai 15, mwaka huu kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Timu
hiyo ambayo kwa mwaka huu imecheza mechi tisa za kimataifa na kushinda
mitano; kutoka sare miwili na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa,
itakuwa na kikosi cha wachezaji 24.
……………………………………………………………..…………… …………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment