KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, February 25, 2013

MAMA SALMA AANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI RUKWA.

 Mke wa Rais naMwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na mkuu wa Mkoa wa Rukwa mara tu baada ya kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akivishwa skafu na chipukizi mara baada ya kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
 Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea salamu ya heshima kutoka kwa chipukizi wa mkoa wa Rukwa waliofika uwanja wa ndege kumlaki. Mama Salma Kikwete yupo Mkoani  Rukwa kwa ziara ya siku tatu.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Pamoja na mambo mengine Mama Salma atakabidhi vifaa vya tiba katika hospitali ya Mkoa wa Rukwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Pamoja na mambo mengine Mama Salma atakabidhi vifaa vya tiba katika hospitali ya mkoa wa Rukwa. (PICHA NA JOHN LUKUWI)

No comments: