KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, May 1, 2013

MTANZANIA AOMBEWA ITC ACHEZE NORWAY

Shirikisho la Mpira wa Miguu Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili aweze kucheza mpira nchini humo.

NFF inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini Norway.
AZAM YAENDELEA KUJINOA MOROCCO
Timu ya Azam ambayo iko jijini Rabat kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabati ya huko inaendelea vizuri na mazoezi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi wa Azam FC, Jaffer Idd maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Mei 4 mwaka huu). Jaffer Idd anapatikana kwa namba


No comments: