Mikoa
18 kati ya 27 ya kimpira tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya
usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu
tatu za juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014). Ligi ya FDL ina jumla ya
timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu ni
Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa na Morani FC ya
Manyara.
Mabingwa
waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar
es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends
Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United
(Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Wengine
ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe
(Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1),
Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero
ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Kila
klabu inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati
usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya
Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF
inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya
ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment