MJUMBE wa Halmashauri Kuu ta CCM Taifa, wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akitoa semina ya ujasiriamali wa kilimo cha alizeti kwa Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake (UWT) wilayani humo hivi karibuni.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na wananchi wa kata za Bungu, Lulindi na Dundila katika harakati za kuhamasisha kilimo cha alizeti wilayani humo. Kulia ni Katibu wa UWT wilayani humo, Sophia Kupe na Mwenyekiti wa CCM kata ya Bungu, Rashid Mavua.Kushoto ni Diwani wa kata ya Kwadelo, Kondoa, Omari Kariati.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akimtambulisha Diwani wa kata ya Kwadelo, Kondoa, Alhaji Omari Kariati kwa wananchi waliohudhuria kupata elimu ya kilimo cha alizeti. Mkutano huo ulifanyika katika kata ya Bungu wilayani humo na diwani huyo alishiriki katika kutoa ushuhuda wa namna kilimo hicho kinavyoweza kuwanufaisha wananchi wa wilaya hiyo kutokana na kata yake kunufaika nacho.
BAADHI ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kuwahamasishwa kulima alizetil katika ya kata ya Magoma wilaya ya Korogwe Vijijini, wakinyoosha mikono kukubali kwamba watalima zao hilo baada ya kupata elimu ya zao hilo. Mkutano huo uliitishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilayani humo, Dk. Edmund Mndolwa ambaye amejitolea kuhamasisha wananchi kulima alizeti ili waweze kuondokana na umasikini.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Edmund Mndolwa akipata soda na mihogo baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Magoma Wilayani humo kuwahamasisha kulima alizeti.Kulia ni Diwani wa Kaya hiyo, Khadija Mshahara na kushoto ni Diwani wa kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa, mkaoni Dodoma.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk Edmund Mndolwa akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa, Alhaji Omari Kariati wakati wakikagua moja ya shamba la alizeti katika kata ya Mnyuzi wilayani humo.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akicheza pamaoja na kikundi cha kina mama katika kijiji cha Hale, kata ya Mnyuzi walipomlaki wakati wa kufika eneo la mkutano uliofanyika katika soko kuu la kijiji hicho.
NA MWENDISHI WETU, KOROGWE
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujikita katika kilimo cha alizeti ili kiweze kuwakomboa kiuchumi.
Dk. Mndolwa alieleza kuwa mazingira
ya wilaya hiyo na mkoa wa Tanga kwa jumla, yanahimili kilimo cha
alizeti hivyo kama wananchi watakithamini na kulifanya zao hilo kuwa la
biashara kwao watanufaika haraka.
Akihamasisha wananchi kutoka
vijiji, kata na tarafa za wilaya hiyo juzi, Dk. Mndolwa aliwahakikishia
wananchi hao kwamba kilimo cha alizeti hakitaweza kuwatupa kutokana na
utafiti wa kisayansi kuthibitisha ubora na manufaa ya zao hilo.
“Kwa
vile chama chetu kinahimiza kilimo kwanza , chini ya mwenyekiti na rais
wetu, Jakaya Kikwete kamati kuu ilipitisha uamuzi wa alizeti kuwa zao
la biashara katika wilaya yetu na mimi nimeagizwa na chama kuhimiza zao
hili ili muweze kunufaika nalo,
“Lakini
kabla ya kufikia hatua hii ilinibidi kata ya Kwadelo, Kondoa kujifunza
namna ya kulima alizeti na namna gani mtaweza kunufaika nayo, kwa hiyo
limeni zao hili ambalo kwa wilaya yetu tutanufaika zaidi kuliko Kondoa,
ambao wanategemea msimu mmoja wa mvua tofauti na sisi tunaopata misimu
miwili,”alieleza.
Akifafanua manufaa makubwa ya zao hilo, Dk. Mndolwa alisema kwamba ekari moja inaweza kutoa magunia 12 hadi 18 na kwa maana hiyo wastani wa ekari moja unaweza kupata lita 300 za mafuta ambazo ni sawa na thamani ya sh.450,000.
Alieleza pia kuwa mkulima akiamua kulima misimu yote miwili kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo, atakuwa
na uhakika wa kuingiza sh.900,000 kwa ekari, kitu ambacho kitawasaidia
kupata mapato makubwa kama wataweka juhudi za kulima mashamba makubwa
zaidi.
Dk
.Mdolwa alisema mafuta ya zao hilo ndiyo yenye soko kubwa kwa sasa,
hivyo kuwataka wananchi hao kutokuwa na wasiwasi juu ya upatikaji wa
soko na badala yake waunge mkono kilimo hicho ili kiweze kuwanufaisha.
Katika
kuonyesha kwamba anataka wananchi hao walime alizeti, Dk. Mndolwa
aliahidi kuwalimia vijana ekari tano kila kata, ambao watajiunga katika
vikundi vya watu watano ili kuanza kupata shamba darasa.
Akitilia mkazo juu ya umuhimu wa kilimo hicho, Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa, mkoani Dodoma, Omari Kariati alisema kuwa wakati wananchi wa kata yake wanaanza kulima zao hilo hawakuanza na mafanikio ya moja kwa moja lakini kwa sasa wamefanikiwa.
“Kwa
sasa mkulima mdogo katika kata yangu analima ekari 50 na kuna watu
wanalima mpaka ekari 200, kitu ambacho kimefanya wananchi wa kata ya
Kwadelo kutokuwa na shida ya fedha badala yake wanashindana kimaendeleo,
“Hata vijana na kina mama mkiamua mnaweza kwani katika kata yetu, kundi lenu
ndilo lenye kumiliki uchumi mkubwa na hawana muda wa kupoteza zaidi ya
kuzungumzia namna ya kuboresha kilimo chao cha alizeti, kitu ambacho
mnatakiwa kukifanya pia watu wa Korogwe Vijijiji,”alieleza.
Kariati alisema wakati wanaanza kulima, kata
yake ilikuwa na matrekta matano lakini kutokana na manufaa makubwa ya
kilimo hicho kata ina matrekta 65, ambayo yanamilikiwa na wananchi
wenyewe.
Katika
kuhamasika na kilimo hicho, wananchi wa vijiji, kata na tarafa
zilizotembelewa walikubali kuungana kulima zao hilo ingawa kilio chao
kilikuwa tatizo la ukosefu wa ardhi ya kutosha, tatizo ambalo Dk.
Mndolwa aliahidi kulishughulikia kwa kushirikiana na viongozi wa
serikali.
No comments:
Post a Comment