Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana kitabu cha kampeni ya Lishe
Tanzania baada ya kukizindua katika bustani ya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.
Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na
Taasisi ya Chakula na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe
na maendeleo yake nchini katika uzinduzi wa kampeni ya lishe
nchini katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni
Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment