Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa,
akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,
Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa
kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda.
Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa,
wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika
Viwanja vya Ifunda.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa
CCM, Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na
watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na
mwingine kutobolewa jicho kwenye kampuni zinazohusu udiwani na Ubunge,
katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema,
wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika
Viwanja vya Ifunda.
Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda.
Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa
uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda.
Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye
misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru
msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga (PICHA NA BASHIR NKOROMO)
No comments:
Post a Comment