Wananchi
wa mji mdogo wa Kalenga, katika Kata ya Kalenga, Iringa Vijijini,
wakimshangilia kwa bashasha mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo
la Kalenga, Godfrey Mgimwa, alipokuwa akiwaaga, baada ya kuhutubia
mkutano mkubwa wa kampeni katika kijiji hicho.
Wananchi
wa mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini wakiwa katika hoihoi na
nderemo kumkaribisha mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la
Kalenga, alipofika kuhutubia mkutano wa kampeni.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akihutubia mkutano wa kampeni za CCM
za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, uliofanyika katika mji mdogo wa
Kalenga, Iringa Vijijini.

Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, akimnadi mgombea ubunge kwa
tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo
katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini.
Mgombea
ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Godfrey Mgimwa, akihutubia
mamia ya watu kwenye mkutano wa kampeni leo katika mji mdogo wa Kalenga,
Iringa Vijijini.

Mgimwa
na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, wakisalimia
wananchi baada ya mkutano wa kampeni katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa
Vijijini.
Mgombea
ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga,
Godfrey Mgimwa, akiwa amebebwa na Wananchi alipowasili kuhutubia
mkyutano wa kampeni katika kijiji cha Ipamba, Tosamaganga.
Sista
Paula Msambwa mwenye umri wa miaka 73, akimbusu kwa furaha, mgombea
ubunge kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, mgombea huyo alipowasili
kuhutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Ofisi ya CCM Tosamaganga,
Iringa Vijijini leo. Sista Paula alisema, aliwahi kuwa mwalimu wa Baba
wa mgombea huyo, Marehemu Dk. William Mgimwa miaka 50 iliyopita katika
shule ya Tosamaganga.
Sista
Paula Msambwa akimtakia kila la kheri ikiwemo kushinda katika uchaguzi,
mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa, alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye
mkutano huo.
Mgombe
ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,
akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Ipamba, Tosamaganga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia mkutano wa kampeni kwenye kijiji hicho.
Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akipokea kadi ya Chadema
kutoka kwa Said Omary Mbilinyi ambaye amerudi CCM kwenye mktano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye kijiji hicho.
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mtela
Mwampamba
akihutubia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kijiji cha
Ipamba, Tosamaganga, leo na kuwataka wananchi kutambua kuwa huduma
ambazo huwa wanaziona kwa kupelekwa kwao na serikaloi zina uhusiano
mkubwa na CCM.
Katibu wa CCM
Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia mkutano wa kampeni
uliofanyika Kijiji cha Tosamaganga wakati wa kumnadi mgombea wa kiti cha
ubunge kupitia CCM, Godfrey Mgimwa.
Hizi
ni shamrashamra za wananchi zilizohanikiza wakati mgombea ubunge kwa
tiketi ya CCM jimbo la kalenga, Godfrey Mgimwa, alipowasili katika
kijiji cha Ipamba, Tosamaganga.
Wafanyabiashara
katika Kijiji cha Ipamba, Tosamaganga wakiwa wamecha vibanda vyao vya
biashara na kwenda kumsikiliza mgombea ubunge jimbo la Kalenga kwa
tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa alipohutubia katika kijiji hicho.
Helen
Msambwa, wa kijiji cha Ipamba, Tosamaganga, akiandaa samaki, huku
akifuatilia kwa karibu hotuba ya mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo
la Kalenga , Mgimwa alipohutubia kwenye eneo hilo. (Picha zote na
Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog)
No comments:
Post a Comment