Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani
wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti
uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na
Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh.
milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha
hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa
kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu
itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na
kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za
watazamaji hao.
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile
TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba
idhidi ya kutumia uwanja huo.
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na
wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa
la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika
endapo kutatokea uharibifu.
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa
baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya
mechi.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
No comments:
Post a Comment