Mamia ya akina mama na wananchi wa Jiji la Mwanza wakishiriki katika
sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa
saratani ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Nyamagana ambapo Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.

Ngoma
ya asili ya kabila la Wasukuma ya Bugobogobo ikichezwa kwa umahiri mkubwa hata
kumfanya Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe
hiyo kushuka jukwaani na kuicheza na baadaye kumzawadia mtoto wa kikundi hicho kutoka Mji wa Magu wakati
wa sherehe za uzinduzi wa upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika
katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza.

Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete
akizindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi wakati wa kilele cha siku ya
wanawake duniani katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko
Mwanza.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango
wa kizazi aliwakabidhi Waganga wakuu wa mikoa ya Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara
vifaa vya kupima saratani hiyo. Pichani
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Valentino
Bangi mkoba wenye vifaa vya upimaji.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory Masalu kutoka
hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima akina mama katika kituo
cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza mara
baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana
na kutembelea kituo hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima.
Mamia
ya wanawake wa Mwanza walijitokeza kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi
kama wanavyoonekana katika picha iliyopigwa katika kituo cha Afya cha Buzuruga
huko Ilemela.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzaia, MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa (wa kwanza
kushoto) akifuatiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa Mwanza Ndugu Magalula Said Magalula,
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Profesa Charles Mapinge na Mama Salma Kikwete
wakiteta jambo wakati walipokitembelea kituo cha afya cha Buzuruga ambacho hutoa
huduma ya kupima saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama.
Mamia
ya wanawake wa Mwanza walijitokeza kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi
kama wanavyoonekana katika picha iliyopigwa katika kituo cha Afya cha Buzuruga
huko Ilemela.
Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia
ya wanawake na wananchi waliokusanyika katika kituo cha Afya cha Buzuruga
kilichoko wilayani Ilemela, Mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa
saratani ya kizazi kwa akina mama.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment