Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu
na Makazi. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi
Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu
na Makazi.Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
imesema kuwa hali ya mfumuko wa bei nchini imeendelea kuwa katika kiwango
kisichobadilika katika kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu kutokana
na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na
sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa
Taifa kwa mwezi Februari 2014 umeendelea kubaki katika kiwango cha
asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Januari mwaka huu.
Amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na
huduma kwa mwezi Februari 2014 imebakia kuwa sawa na ile iliyokuwepo mwezi
Januari huku kukiwa na ongezeko dogo la
upandaji wa bei kwenye baadhi ya bidhaa
na huduma mwezi kwa mwezi Februari 2014 ikilinganishwa na bei za mwezi Februari
mwaka jana.
Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula
na migahawa kwa mwezi Februari umeongezeka hadi asilimia 6.9 kutoka asilimia
6.6 za mwezi Januari mwaka huu huku bidhaa zisizo za vyakula kasi ya ongezeko
la bei ikipungua hadi asilimia 6.3 mwezi Februari 2014 kutoka asilimia 6.7 za
mwezi Januari mwaka jana.
Amefafanua kuwa mwenendo
wa bei za bidhaa za vyakula kama samaki, mbogamboga, ulezi na matunda
zimeonyesha kuongezeka kwa kiwanga kikubwa kwa mwezi Februar ikilinganishwa na
bei za bidhaa hizo kwa mwaka uliopita huku bei za bidhaa zisizo za vyakula za
vitambaa vya suti za wanaume, kodi za pango la kuishi, mkaa, na nauli za bajaji
zikionyesha ongezeko.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi,ameeleza
kuwa kumekuwa na ongezeko kwa asilimia 1.4 ikilinganishwa na ongezeko la
asilimia 1.8 kwa Januari mwaka huu, huku
fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 148.62 kati ya Februari
mwaka uliopita na Februari mwaka huu.
Amezitaja bidhaa
zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na dagaa,samaki wakavu,
mbogamboga na viazi mviringo huku bidha
zisizo za vyakula zikiwa pombe za kienyeji, vitambaavya suruali, viatu vya wazi
vya plastic, mafuta ya dizeli na Petroli
pamoja na huduma za unyoaji na usafi wa nywele.
Aidha kufuatia hali hiyo ya mfumuko wa
bei Bw. Kwesigabo ameeleza kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Februari umeonyesha kupungua na kufikia shilingi 67 na
senti 29.
“Kupungua
kwa thamani ya Shilingi kunamaanisha kwamba, kama mtu alikuwa na uwezo wa
kununua bidhaa kwa Shilingi 100 mwaka jana, basi kwa mwaka huu itampasa aongeze
zaidi ili aweze kununua kitu kama kile kile, kwa mfano badala ya shilingi 100
inabidi atumie Shilingi 132”
No comments:
Post a Comment