Mwezeshaji
wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama Ndugu
Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE (Forum For African Women
Educationalists-Tanzania Chapter) akitoa moja ya mada zake mara tu baada ya
ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo shuleli hapo.
Picha ya
pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Elimu katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi
Alawi akifungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama. Waliokaa kushoto kwake ni Ndugu Obeth Mwakatobe, Makamu Mkuu wa Shule akifuatiwa ni
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE na Kulia
kwa Mgeni rasmi ni Ndugu Philomena Marijani kutoka WAMA. Mafunzo hayo ya siku
tano yalifunguliwa rasmi tarehe 15.9.2014 na yameandaliwa na Taasisi ya WAMA wakishirikiana
na UNICEF.
Baadhi
ya walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungunzi wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo walimu haokatika masuala ya jinsia na stadi za maisha. Hotuba hiyo
ilikuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi (hayupo pichani).

Mkuu wa
Kitengo cha Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
WAMA, Ndugu Philomena Marijani akiwakaribisha walimu na wageni waalikwa wakati
wa sherehe ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya
Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati huko Wilayani
Rufiji yaliyofanyika shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment