KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, May 30, 2015

Kaa tayari kwa 'Movement' mpya ya WBTA na Tanzania mpya!!!

Monika & Us_00000 copyMiongoni mwa viongozi waandamizi wa WBTA, ambao ni mapacha, Frank na Francis (kulia). Kushoto kwao ni mdogo wao, Monica Ntevi.
WBTA
Ni harakati zilizoanzishwa na vijana watatu Frank & Francis Ntevi na Eben Had, ambao wote ni wanafunzi wanaosoma chuo kikuu UDSM, kwa lengo la kuwanyanyua, kusapoti wasomi wote wenye moyo na Sanaa.
Kwa sasa wameanzia ndani ya UDSM, ikiwemo wameanza kusaidia kutoa sapoti kwa UDSM X BAND kwa kuwatengenezea albamu art kwa kushirikiana na mwanafunzi mwingine Papushka ambaye naye yupo kwenye harakati hizo kwa kufaanya video.
Katika haarakati hizo, muunganiko wa wasanii wa chuo kikuu UDSM ALL STARS, wameachia wimbo unaitwa ‘Tanzania mpya’ uliotoka hivi karibuni na pia wapo katika hatua za kutoa video ya wimbo huo.
..Bado haijaanza kupigwa kwenye vituo vya radio kwa sababu wanasubiria video yake kwaza.
“Kwa sasa tunasubiria video hivyo itakapotoka video hivi karibuni ndipo tutakapoachia wimbo huo kwenye vituo mbalimbaali” alieleza Frnacis.
Wimbo huo wa Tanzania mpya umerikodiwa Afrocentrik production ya Ubungo, Mabibo Hostel jijini Dar es Salaam chini ya Producer Davy Machords.
Wimbo huo umetolewa kwa sababu unaelezea kuhusu mtazamo wa Tanzania mpya ikiwemo harakati za kupambana na mauaji ya albino, ufisadi, miundombinu mibovu na matatizo yote ya Tanzania na nama ya Tanzania mpya inatakiwa iwe vipi.
Mtazamo wa Tanzania mpya bila mauaji ya albino, ufisaidi, miundombinu mibovu unyanyapaa, rushwa, na vitu vingi.
Kwa sasa ina wanachama 24 ambao wote ni wanafunzi wa UDSM, na wanavipaji tofautitofauti ikiwemo wanamuziki, models, watunzi wa filamu, muziki, waigizaji, watunzi mashahiri,dansa, Digital Artist.
Aidha, wanatarajia kuelekea kwenye vyuo vyote vya Tanzania kuendeleza movement hii ambapo pia tunatarajia kufanya tamasha moja kubwa wanafunzi wenye ujuzi na sanaa kubwa.
ONE SOCIOLOGIST WBTABaadhi ya 'Members' wa WBTA ..
P Icon JAZZ New
QuizO ARTIST
Renney NOVELIST
Sweesh4Real MUSICIAN
TJ_00000
We Belong To Art
'WBTA'
It’s a movement initially started by 3 Colleges, Frank Ntevi, Francis Ntevi and Ebenhad Osward based on University of Dar es salaam artists, Generally the movement aimed to reunite, support and ignite the students with passion on Art. On Contrary, the artists (Musicians) based on UDSM, came with an idea to change the whole set perspective about Tanzania and the Optimistic ideal Tanzania
Tanzania Mpya is the title of the song, produced under Afrocentric production, Davy Machord as the Leading Producer. The song featured almost the whole set artists of University of Dar es salaam, Likes of Jo summit, T-Gwan, Nelina, Bobby Ray, Tracy J, Jimmy Mo, Safe, My self, Tomino, Penny, C rex. Regardless of their specialization. The song speaks about the Optimistic about the Future Tanzania, and in the process what should be done. With also on the verge to release track officially, and the Music video under Directorship of Papushka and his team sooner.
Urging Tanzanians to listen to the track and see what the UDSM students thoughts of.
WBTA 2 Logo HD 2
# 5_00000_00000
WBTA season 2_00000
WBTA Tshirt Tangazo_00000
David JUJITSU
TudoR NOVELIST

Wednesday, May 27, 2015

VETA YASAINI MAKUBALIANO YA MSAADA NA SERIKALI YA AUSTRALIA .

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam.Wengine Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames (wa pili kushoto) Balozi wa Australia nchini John Feakes na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba.  
  Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames.
 Wageni waliohudhulia  sherehe ya kusaini makubaliano.
 Wageni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi (kulia) na Naibu waziri Wizara ya Afya na Utalii wa Australia Magharibi Dk,Kim Hames (kushoto) wakitia saini makubaliano wakishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba(kulia) pamoja na Balozi wa Australia nchini John Feakes.
 Wakipongezana baada ya kusaini.
 Wakiwa katika picha ya pamoja viongozi walioshuudiwa kutia saini makubaliano hayo.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepata msaada kutoka Serikali ya Australia kupitia Idara ya Biashara na Mambo ya Nje  (DFAT) wa kutengeneza mfumo wa namna ambavyo VETA itakuwa ikishirikiana na viwanda pia waajiri mbalimbali katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi. Mfumo huo utakuwa ndio mwongozo wa kuainisha utaratibu wa mafunzo ya ufundi na viwanda au sekta mbalimbali za uchumi mfano sekta ya madini, gesi, utalii n.k.
Mfumo huu utatengenezwa na wataalamu kutoka Australia na Serikali ya Australia imekubali kutoa fedha kiasi cha TSh. 330 milioni kwa ajili ya kazi hiyo.
Manufaa ya mfumo huo kwa VETA itakuwa:-
1)    Kuimarisha mashirikiano na viwanda au waajiri mbalimbali ili kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana na mahitaji ya soko la ajira.

2)    Utaboresha viwango vya mafunzo yanatolewa na viwanda.

3)    Utapunguza mzigo unaobebwa na Serikali katika kugharamia mafunzo ya ufundi stadi kwa vile viwanda vitakuwa na fursa ya kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalamu wa kufundisha.

4)    Pia walimu wa VETA watakuwa wanajengewa uwezo maana mfumo utawawezesha kufanya mazoezi ya vitendo (practical training) viwandani mara kwa mara ili kunoa ujuzi wao.

5)    Mashirikiano haya yatafungua fursa nyingi za ushirikiano na Taasisi mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi nchini Australia hasa tukizingatia kuwa Australia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mafunzo ya ufundi stadi.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saidni leo 27 Mei, 2015 kati ya VETA na Idara ya Biashara na Mambo ya Nje ya Australia katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam

Balozi wa Australia Mheshimiwa John Feaks na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi walisaini makubaliano hayo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia ya Magharibi, Bw. Kim Hames na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Tanzania), Bi. Consolata Mgimba.

Balozi wa Australia alisema kuwa, Serikali yake imeamua kuisaidia VETA ili kuimarisha taasisi za elimu na mafunzo ya ufundi na hivyo kuwa na uwezo wa kutoa wahitimu wenye ujuzi wa kutenda kazi katika eneo la gesi, mafuta na madini.

Alisema kuwa msaada huo utalenga zaidi katika kugharimia ushauri wa kitaalam kwenye kuandaa mitaala na kujengea uwezo walimu wa mafunzo ya ufundi stadi.

Australia imefurahi sana kuisaidia VETA katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa Watanzania wako katika nafasi nzuri za kutumia na kunufaika na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, gesi na mafuta nchini mwao,” alisema.

Upatikanaji wa wafanyakazi wenye ujuzi wa aina mbalimbali unayapa makampuni makubwa ya uwekezaji fursa ya kuajiri wafanyakazi kutoka ndani ya nchi na hivyo kuwanufaisha wao wenye makampuni na jamii ya ndani, kukuza uchumi wa nchi, hususani kwa kuwapatia wananchi ajira na vipato,” alisema Feakes.

“Tukiwa na uwezo na uzoefu mkubwa katika mafunzo ya ufundi stadi kwenye eneo la mafuta, gesi na madini, tuko radhi kuisaidia Tanzania kunufaika na sekta hiyo,” aliongeza.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Consolata Mgimba aliishukuru serikali ya Australia na kusema msaada huo utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kuajirika, utaongeza tija mahali pa kazi na kuchochea ukuaji wa viwanda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA alisema kuwa pamoja na kupata msaada wa kifedha, VETA inatarajia kunufaika kwa kiasi kikubwa na utaalam na uzoefu kutoka Australia kwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na ujuzi mkubwa kuhusu ushirikiano kati ya taasisi za elimu na mafunzo ya ufundi  kwa upande mmoja na viwanda kwa upande mwingine.

Alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuboresha mfumo wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.

“Kuwa na mfumo wenye ushirikiano kati ya viwanda na taasisi za mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu sana. Ni kupitia mfumo huo ambapo kunakuwa na uhakika wa kutoa rasilimali watu yenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya waajiri, inahakikisha ubora na inawahakikishia wahitimu kuajirika”, Alisema Mhandisi Moshi.

Mfumo huo pia unaweza kuisaidia serikali kupata ahueni ya kugharimia elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa kuwa wenye viwanda wanaweza kuchangia katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi.


Kwa mawasiliano zaidi

Sitta Peter
Meneja Uhusiano
Barua pepe: speter@veta.go.tz
Simu: 0767920019/0652226688

MAOMBI YA MCHANGO WA UJENZI WA MSIKITI.

Katika Maisha yetu Wanaadamu Ibada ni Jambo Muhimu saana.
Uzuri , Usafi wa sehemu ya kuabudu ni Moja katika mambo mazuri yenye kupendeza katika kila Nafsi ya Binaadamu.

Katika Nyumba (Msikiti)  huu , Ndugu zetu wanafanya Ibada ya Swala 5 kwa siku , Msikiti huu upo Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Mlamleni Kitongoji cha Kimbangulile.

Wenzetu wameanza kwa Nguvu zao  Ujenzi wa Msikiti kama Mnavyo uona.
Jitihada nyengine wameweza kuwa na Matofali yasiyo pungua 300 kwa Ajili ya kuanza Ujenzi Mpya.

Ukiwa Umeguswa na hili tunaomba kutoka kwako MCHANGO WAKO WA VIFAA VYA UJENZI.

Kwa Mwanzo Tunahitaji
1.Cement
2.Tofali
3.mchanga
4.Vifaa vya Kuchimbia Majembe, Panga , chepe N.k

Maazimio yetu tuanze Ujenzi pale tu tutakapo pata uwezo wa kulifanya hili.

Tunawakaribisha mtembelee eneo la tukio kwa wale ambao Mtakuwa na  Na Muda wa kufanya hivyo.

Michango yenu tunaomba muwasilishe kwa Namba ya Simu.
0715800772( Tigo Pesa ) GHALIB MONERO.

Kwa wale waliopo Nje ya Tanzania : WESTERN UNION : GHALIB NASSOR MONERO

Waliopo KENYA tafadhali wasiliana ALI BAJIY NASOR no' 0725113783 M-PESA.

More Update kuhusu Michango ya Msikiti huu Tafadhali Tutembelee : facebook : Kijana wa Kiislam Dsm or Whatssap Number : +255689604780

Au Piga Simu : +255715800772

Tunawashukuru kwa Michango yenu na Ubalozi wenu Mzuri wa kuitangaza kheri hii .
WABILLAHI TAUFIQ WENU KATIKA UTUMISHI WA DINI KATIKA JAMII.
GHALIB N MONERO.

Tuesday, May 26, 2015

Mfumo DUME.


AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU.


Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
 Aki na Ukwa wa Bongo wakipiga kazi ...
 Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels

Wasanii wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.

Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.

Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.

Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.

"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania.

   Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Mabalozi wa Tanzania unaofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unajadili kwa kina namna ya kutekeleza dira mpya ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya Uchumi na Diplomasia Duniani na kuleta tija nchini.
 Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wakati wa mkutano wa mabalozi wa Tanzania.Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Watatu Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje Mh.Bernard Membe,Wanne kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula(Picha na Freddy Maro).

JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA.


Msanii Juma Nature 'Kiroboto' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini  pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said Christopher 'Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii  Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri 'Msagasumu' na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix 'Fredwayne' Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher 'Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

............................................................................................................
                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                              KOMAA CONCERT

Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya msanii JUMA NATURE  maarufu kama kiroboto pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi  jumamosi hii ya  tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala,  kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo  Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Aidha, mashabiki watapata burudani kutoka kwa kiroboto  ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na  Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.

Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.

Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya.

Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu sisi tunaamini Muziki unaongea. 
IMETOLEWA NA, DENIS SSEBO,
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM.

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MABENKI YA AKIBA DUNIANI (WSBI) KANDA YA AFRIKA.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa mabenki ya Akiba Duniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia kesho jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa mabenki ya Akiba Duniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia kesho jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi na kushoto ni Mundakweli Kaniki Meneja Mwandamizi wa Mipango Mkakati ya TPB. Mkutano huo utashirikisha zaidi ya washiriki 100 kutoka nchi mbalimbali Afrika na viongozi wa Dunia wa Taasisi hiyo ya WSBI ambapo pia TBP ndio Benki mwenyeji wa mkutano huo.

Sunday, May 24, 2015

Rais Kikwete atoa Msaada kwa Timu ya Kilimani Sports Club mjini Dodoma.

Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi timu ya soka ya Kilimani Sports Club jezi na mipira katika ikulu ndogo ya mjini Dodoma leo asubuhi.Rais Kikwete alitoa msaada kwa timu hiyo baada ya kuwakuta vijana hao wakifanya mazoezi bila zana bora katika uwanja wa mpira ulioko eneo la Kilimani karibu na ikulu wakati Rais alipokuwa akifanya mazoezi ya kutembea katika eneo hilo.Wakiongea mara baada ya kupokea msaada huo vijana hao walimshukuru Rais Kwa moyo wake wa upendo na nia yake ya kukuza vipaji kwa vijana na kuahidi kufanya vyema katika ligi ya Wilaya ya Dodoma mjini (Picha na Freddy Maro)

Six MENO.


Saturday, May 23, 2015

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR NDUGU SEIF SHARIFF HAMAD.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo, Jumamosi, Mei 23, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Ikulu Ndogo, Dodoma. Rais Kikwete akimwaga Mheshimiwa Hamad baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
(Picha na John Lukuwi, Maelezo).

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED.

 Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae ,Lets Get Married iliyichezwa na wachina na kutafsiriwa kwa kiswahili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar e Salaam jana. Kulia ni Ofisa kutoka ubalozi wa China, ambaye alikuwa ni mkalimani wa balozi huyo, Yetianfa Attache.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.
 Maofisa wa Kampuni ya StarTimes wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Warembo wa StarTimes wakiwa tayari kwa zoezi la kuzindua Tamthilia hiyo. Kutoka kulia ni Hadija Saidi, Nyachilo Bunini na Fausta Mushi.
 Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta'  (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.

Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane 'Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.

"China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta  ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa" alisema Balozi Dong.

Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.

Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.

Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane.