Uongozi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na Uongozi
wa klabu ya Simba SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi
wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki
kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na
klabu ya Simba.
Katika
kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya
mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa
wa Simba SC.
Kwa
pamoja pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano
mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
TFF
imevitaka vilabu kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka
mifumo mizuri ya uingiaji mikataba. TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs). Aidha TFF imewataka wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.
TFF
itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka
mazingira sawia kati ya pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yamefanyika leo tarehe 9 Juni 2015 na kusainiwa na:-
- Collin Frisch - Simba SC
- Ramadhan Singano - Mchezaji
- Mussa M. Kissoky - SPUTANZA
- Mwesigwa J. Selestine - Katibu Mkuu - TFF
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment