Catherine
Sungura, MOHSW- Arusha.
Zaidi
ya dozi milioni52 za dawa zinazotibia magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele ya matende, vikope, mabusha,minyoo ya tumbo, kichocho na usubi
zimetolewa na Serikali kwa watanzania milioni 21 katika kipindi cha mwaka 2014.
Takwimu
hizo zimetolewa jana jijini hapa na Katibu Mkuu wizara ya Afya na ustawi wa
jamii Dkt Donan Mmbando katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa nne
wa kazi kati ya wizara hiyo na wadau wanaofadhili mpango huo iliyosomwa
kwa niaba yake na mkurugenzi wa idara ya huduma ya kinga katika wizara hiyo
Dkt.Neema Rusibamayila.
Dkt.
Rusibamayila alisema katika kipindi cha mwaka 2014/2015, mpango huo ulifanikiwa
kuwafikia watanzania katika wilaya 110 na mikoa 17 ya Tanzania ikiwemo
wanafunzi katika ngazi za shule ya msingi
na watoto wenye umri wa kwenda shule.
Hata
hivyo alisema katika kwa mwaka huu mikoa minne zaidi inayokabiliwa na tatizo la magonjwa hayo
imelazimika kuongeza idadi ya mikoa
katika mpango huo ikiwemo mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Simiyu, , Geita .
"Leo
ikiwa tunakutana hapa tunajivunia kazi tuliyoifanya kwa kuwa tayari Takwimu
zinaonyesha wilaya 6 hazihitaji dawa za matende ugonjwa huo umeshamalizika,
ugonjwa wa trakoma tulifanya utafiti wa awali wilaya31 tumegundua ni wilaya moja
tu ya Chunya Mkoani mbeya ndio imekuwa ikihitaji dawa ,Vilevile thathmini
ya trachoma iliyofanyika katika wilaya 28
imeonyesha kuwa wilaya 19
zimefaulu hivyo kutohitaji ugawaji dawa wakati 9 zitaendelea na ugawahji
dawa za Zithromax,"alisema.
Kwa upande
wake Mratibu wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka wizara
ya Afya na ustawi wa jamii Dkt. Upendo Mwingira alisema mpango huo wa Serikali
umekuwa na faida nyingi kuliko changamoto.
"Baadhi
ya changamoto ni pamoja na utoaji huduma
kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji hasa kwa wale ambao wamekwisha athirika na
magonjwa haya hasa vikope na matende, tunawasiliana na wadau wetu ili kuwapatia
huduma hii, lakini pia kuna tatizo la uelewa ijapokuwa wengi wamekuwa waelewa
baada ya kutumia mbinu mbalimbali za kuwaelimisha umuhimu wa zoezi tunalokuwa
tunafanya,"alisema.
Kwa
upande wake Kaimu mganga mkuu wa Mikoa wa Arusha Dkt. Omar Chande, alisema
zoezi la ugawaji wa dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa hayo limeenda vizuri
na matokeo yanaonyesha zaidi ya asilimia 85 ya
watoto wenye umri wa kwenda shule walipata dawa za kichocho na minyoo mnamo mwezi Mei
2015. utafiti wa awali umeonyesha kuwa
wilaya zote zimeathiriwa na baadhi ya magonjwa hayo.
No comments:
Post a Comment