Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis
kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika
siku ya jumamosi nchini humo.
Mchezo huo wa marudiano kuwania
kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa
siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira
ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kocha mkuu wa Taifa
Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri
na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini
Uganda.
“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi,
vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya
vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.
Taifa
Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa
shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji
20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.
Aidha Mkwasa amesema
ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili -
Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa
marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.
Stars
imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya
mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya
saa 10 jioni.
FDL KUCHEZWA MAKUNDI MATATU 2015/2016
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi
matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mfuko
huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao cake
kilichofanyika mjini Zanzibar.
Timu ya kwanza katika kila kundi
la ligi hiyo itakayoanza Septemba 12 mwaka huu itapanda kucheza Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi
ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL)
kwa msimu wa 2016/2017.
Kundi A linaundwa na timu za African Lyon
FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers
FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal
Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam
na Polisi Dodoma.
Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC
(Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC
(Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting
(Pwani).
Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC
(Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC
(Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).
U15 YAREJEA DAR
Kikosi
cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo
kinarejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mbeya ambapo jana
kiliibuk ana ushindi wa ushindi wa mabao 4-1.
U15 ambayo
inaandaliwa kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za vijana chini ya
miaka 17 barani Afrika kilikua na ziara ya michezo ya kirafiki miwili
jijini Mbeya ambapo katika mchezo wa awali pia kiliibuka na ushindi wa
mabao 3-0.
Mara baada ya kurejea leo jioni jijini Dar es salaam,
kambi ya timu hiyo itavunjwa mpaka watakapokutana tena mwisho wa mwezi
ujao kwa ajili ya kuelekea visiwani zanzibar kwa jili ya michezo ya
kirafiki.
Lengo la michezo hiyo ya kirafiki ni kutoa nafasi ya
kocha Bakari Shime kutambua uwezo wa vijana wake na kuongeza wachezaji
wengine katika kikosi hicho kisha kuandaa kikosi bora kitakachoshirki
kuwania kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Madagascar mwaka
2017.
PRESS CONFERENCE
Baraza la Vyama vya Soka kwa
Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho siku ya jumatano
kupitia kwa viongozi wake wa ngazi za juu, wataongea na waandishi wa
habari saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo
Karume.
Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment