KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, January 21, 2017

NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mst. Zanzibar, Hamid M. Hamid (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa NEC walipotembelea vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Dimani kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika Jumapili, Januari 22, 2017.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar.  Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emmanuel Kawishe (katikati) na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani, Idaya Seleman Hamza.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R), Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani. Kulia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani, Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani, Idaya Seleman Hamza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R). Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Emmanuel Kawishe mara baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage (kushoto)  akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa  pili kutoka kushoto) na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la Dimani. Katikati ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo la Dimani, Idaya Selemani Hamza, Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Emmanuel Kawishe (wa pili kutoka Kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya  Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mhandisi Isack Manyiri. 

No comments: