Leo tarehe 14th Desemba 2012, African
Barrick Gold Maendeleo Fund inazindua rasmi mpango “Nightwatch”
utakaofanyika katika Kanda ya Ziwa. Mpango huu wa NightWatch, umeandaliwa na Malaria No More kwa kushirikiana na Mradi wa Lalela, ikiwa ni kampeni inayoshirikisha vyombo vya habari inayolenga
kuwakumbusha watu juu ya umuhimu wa
kulala kwenye vyandarua
vyenye dawa ya kudumu ili kujikinga na malaria. Afrika Barrick Gold Maendeleo Fund
na Tanzania House
of Talent zinaungana kwa pamoja
kutekeleza mpango huu katika unaoanzia Kanda ya Ziwa
kufikia jamii zinazoendelea
kuathirika na ugonjwa huu..
Watekeliezaji mkuu katika mpango huu, Tanzania House of Talent
(THT) kwa sasa wanarusha matangazo katika televisheni ya taifa na redio kama sehemu ya mkakati wake wa Zinduka! Malaria
Haikubaliki! Katika kanda ya Ziwa mpango
unaoungwa mkono na Afrika Barrick Gold Maendeleo Fund
utatumika kama chachu katika kuimarisha
kampeni hii ya kitaifa.
"Tunafurahi kufanya kazi na Tanzania House of Talent, Malaria
No More na Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii katika
kampeni hii ya kitaifa, ili kupambana na malaria ugonjwa unaoendelea kuongoza katika
kusababisha maradhi na vifo katika
Afrika. Hii inadhihirisha umuhimu wa makampuni
na wananchi wote kwa ujumla kushikiana katika kutoa elimu juu ya malaria. Kampeni hii tumelenga Kanda ya
Ziwa sehemu ambayo shughuli zetu za uchimbaji wa madini zinafanyika. " Alisema Deo Mwanyika, ABG Vice President Corporate
Affairs.
Kanda ya Ziwa inakabiliwa na tatizo kubwa la malaria ikilinganishwa na sehemu nyingine za nchi.
Tanzania National Malaria Control Program
(NMCP) imesimamia jitihada za serikali
na washirika wa afya
kwa kutoa zaidi ya vyandarua vyenye dawa ya kudumu milioni 26
miaka 3 iliyopita na pia kuongeza
upatikanaji wa dawa ya ukoko, uchunguzi na
matibabu ya malaria. Ili kuhakikisha kwamba
mafanikio haya yanadumishwa katika kupambana na malaria, NMCP inahimiza na kuunga mkono kampeni za mawasiliano. NightWatch inaimarisha upatikanaji wa taarifa kuhusu
malaria kwa njia mbalimbali,
hivyo inawezesha tabia za
kudhibiti malaria kama vile kulala kwenye chandarua chenye dawa kila usiku,
kwenda kupata matibabu haraka kuwa tabia ya kawaida na inayozoeleka.
Programu ya Nightwatch kwa kanda ya Ziwa
imeshirikisha wasanii maarufu nchini Tanzania kama vile Diamond, Masanja
Mkandamizaji, Mwasiti, Dina Marios, Mheshimiwa Vicky Kamata (Mbunge) na Barnaba
ambao watatumia nafasi yao kutoa ujumbe
nyakati za usiku kuhusu malaria kupitia
vituo vya redio za jamii.
"Lengo kubwa la
kampeni ni kuwahamasisha Watanzania
kuchukua hatua na kujizuia wao wenyewe na watu wengine kutoambukizwa malaria katika jamii
yao. Kupitia kampeni hii, tunatarajia kumwezesha kila
mtu kuchukua hatua na kulinda
wenyewe na familia yake kutokana na
malaria, " alisema Mwasiti, Balozi wa mradi wa
Zinduka. "Kampeni hii
inatarajiwa kujenga harakati nchini
kote, na natumaini yangu kwamba mpango
huu wa NightWatch utaongezea nguvu jitihada ambazo jamii imekua ikifanya katika sehemu wanazoishi."
Ujumbe wa Nightwatch utaanza kusikika Disemba 14,
2012 Passion FM na Kwizera FM
Kwa taarifa zaidi za
kampeni ya NightWatch: http://www.malarianomore.org/what-we-do/tanzania-nightwatch
No comments:
Post a Comment