Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa katika mchezo wa mpira wa miguu wakati wa siku yao ya Michezo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari ya Hindi Dar es Salaam.
Na Mwandishi
Wetu
BENKI ya
Azania ya Tanzania imesema kuwa michezo ni muhimili unaosaidia kuimarisha afya,
kuleta umoja na kukuza utendaji kazi wa watu katika maeneo mbalimbali ikiwemo
sekta ya kibenki.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Bw. Charles Singili,
wakati wa hafla ya wafanyakazi wa benki hiyo ya mwaka 2012 iliyowakutanisha
wafanyakazi wa makao makuu na matawi yake yote yaliyopo Dar es salaam.
Wafanyakazi
hao walishiriki katika michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu, kuogelea pamoja na kucheza
muziki, tukio lililofanyika mwishoni mwa wiki
katika ufukwe wa bahari ya Hindi Dar
es Salaam.
“Hili ni
tukio muhimu sana kwetu kama Benki ya Azania kwa kuwa tunahitaji wafanyakazi
wetu kuwa katika afya nzuri kimwili na kiakili na tunatambua kuwa kupitia
michezo tutaendelea kuwa na wafanyakazi wenye afya nzuri na wataweza kuongeza
juhudi katika utendaji kazi wao na kuleta umoja ndani yetu.
“Matukio
kama haya yanayokutanisha wafanyakazi wetu, yanatusaidia katika kufahamiana
vizuri, kubadilishana mawazo na kutafakari kwa umoja wetu nini tufanye zaidi
katika kuhudumia wateja na kukuza huduma zetu na kuleta tija zaidi katika sekta
ya kibenki,” alisema Bw. Singili.
Alisema kuwa
baada ya kufanyakazi mwaka mzima wakiwa wanahudumia wateja wao na kuwasaidia
kufikia malengo yao kwa kuwapatia huduma za kifedha na za kibenki, benki hiyo
iliona ni vyema kupata japo siku moja ya kushiriki katika michezo na wakati huo
huo kuweza kutafakari kwa pamoja ni jinsi gani benki itaongeza tija katika
kuwahudumia wateja pamoja na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa
ujumla.
“Benki ya
Azania haishiriki katika michezo tu lakini pia inasaidia makundi mbalimbali ya
kijamii katika mahitaji ya kiafya, kielimu na kutoa misaada kwa mayatima na
makundi mbalimbali ya wasiojiweza. Tunatoa michango yetu tukitambua umuhimu wa
makundi haya katika kusaidia kujenga Taifa letu,” mkurugenzi huyo alisema.
Bw. Singili
aliongeza kuwa benki hiyo hutoa misaada hiyo ikiwa ni kama jukumu la benki
katika kuirudishia jamii sehemu ya mapato yake wakati benki inatengeneza faida.
No comments:
Post a Comment