KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, December 14, 2012

CHUO CHA VETA KIPAWA CHAFANYA MAHAFALI YA KWANZA KATIKA TAASISI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)


Mgeni rasmi mjumbe wa Bodi VETA Kanda ya Dar es Salaam,Ndibalema Mayanja,(kushoto) akiwa katika moja ya madarasa.
 Mgeni Ndibalema Mayanja,(wa tatu kulia)akipata maelezo kutoka kwa Kasuma Hilary Nchimbi (kushoto) wa Multimedia na Graphic Design.
 Mgeni Ndibalema Mayanja (mwenye suti) akipata maelezo kutoka kwa Ricky Sambo (kushoto).na Mkuu wa Chuo Eng,Luteganya Lucius (wa pili kushoto)

 Baadhi ya wahitimu na walimu wao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kozi ya Malttimedia and Graphics Design.




Na Mwandishi Wetu

Chuo cha Teknolojia za Habari na MawasilianoVETA KIPAWA cha jijini DSM kimeanzisha mchakato wa kutoa mafunzo ya kina ya wataalamu wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati za jua na upepe ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa nishaTI HIYO NCHINI.
Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi LUCIUS LUTEGANYA amewaeleza washiriki wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho kuwa  hatua hiyo inalenga kupunguza idadi ya wananchi wanaokosa nishati hiyo kwa kutofikiwa na gridi ya taifa ya umeme.
Mhandisi Lutenganya amesema hatua hiyo itasaidia kufikisha teknolojia ya ufuaji umeme kwa nguvu za jua na upepe katika maeneo mengi ya vijijini ambako ukosefu wake husababisha athari nyingi ikiwemo kudumaa kimaendeleo na huduma duni za jamii.
Naye Mgeni Rasmi katika mahafali hayo ambaye ni mjumbe wa Bodi ya VETA Kanda ya DSM bwana NDIBALEMA MAYANJA amesema ni muhimu wahitimu wa fani mbalimbali chuoni hapo katika teknolojia za habari, Mawasiliano, Umeme na Elektroni kuondokana na fikra za kutegemea ajira kutoka serikalini pekee na badala yake kuangalia uwigo wa ajira katika sekta binafsi.
Mathalani Bwana MAYANJA amesema ni muhimu wakatazama soko la ajira kwa kuunganisha nguvu zao na kujiajiri wenyewe na kwenda katika nchi mbalimbali za Maziwa makuu na afrika kwa jumla ili kukabiliana na tatizo la ajira ambalo kwa sasa linakabili karibu asilimia 12 ya vijana nchini
Amesema ni nlazima kuangalia soko la ajira la sekta binafsi kwasababu karibu kila nchi duniani inahimiza kila serikali kuweka mazingira bora ya sekta binafsi kukua na kupanua uwigo waajira ili kuziacha bila mzigo huo.
Awali katika risala yao wahitimu hao wa chuo cha VETA KIPAWA wameiomba mamlaka inayomiliki chuo hicho kuongeza madarasa, vitabu na studio zenye vifaa vya kisasa ili kuwawezesha kuhitimu mafunzo ya teknolojia za mawasiliano kwa vitendo.
Chuo cha Tekonolojia za Habari na Mawasiliano VETA KIPAWA kimeanzisha na serikali ya TANZANIA kwa gharama ya shilingi zaidi ya sh bilioni 3 ikiwa ni msaada kutoka serikali ya Jamhuri ya KOREA kikiwa na uwezo wa kuchukua karibu wanafunzi 1900 kwa mwaka wakiwemo wa kozi ndefu na fupi.

No comments: