Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishangiliwa na watoto wadogo
(chekechea) wa shule ya awali ya Carlton iliyoko Colombo, nchini Sri
lanka wakati Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Madola
walipotembelea shule hiyo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishangiliwa na watoto wadogo
(chekechea) wa shule ya awali ya Carlton iliyoko Colombo, nchini Sri
lanka wakati Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Madola
walipotembelea shule hiyo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,
Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Sri lanka Madame
Shiranthi Rajapakse ambaya pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Shule za
Carlton nchini humo wakati walipokutana kwenye moja ya shule hizo
iliyoko Colombo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa
anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha
nchini Sri lanka.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa
anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha
nchini Sri lanka.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mke wa Waziri wa Mambo ya
Nje wa India Mama Louise Khurshid, na Mama Charlotte Scott, Mke wa
Makamu wa Rais wa Zambia wakipata maelezo kuhusiana na Gangaramaya
temple kutoka kwa Naibu Mkuu wa Temple hilo Van Kirinda Assage
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Kiongozi wa Gangaramaya Temple Van Kirinda Assage.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na wake wa Marais na Wakuu wa
Nchi za Jumuia ya Madola wanaohudhuria mkutano wa Madola mjini Colombo
nchini Sri lanka wwakipokewa na mwenyeji wao Mama Shiranthi Rajapakse
wakati walipotembelea Maonesho ya kazi za mikono (handcrafts) yaliyoko
eneo la Janakala Kendraya katika vitongoji vya mji wa Colombo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Dunya
Liyanage, 8, anayesoma darasa la 3 katika Shule ya Msingi ya Meusnes
iliyoko mjini Colombo wakati Mama Salma na wake wa Marais kutoka nchi za
madola walipotembelea maonesho ya Kendraya.
Wake wa Marais na wakuu wa nchi za Jumuia ya Madola wakimwangalia mama
mmoja wa Sri lanka aliyekuwa akitwanga kwenye kinu wakati
walipotembelea maonesho ya Kendraya huko Colombo.
Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na wake wa Marais kutoka nchi za
Jumuia ya Madola wakiangalia jinsi mwanaume na mwamamke wakishirikiana
kufinyanga vyungu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mama Louise Khurshid,
Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India pamoja na Mama Penehupifo
Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia wakitembelea sehemu mbalimbali za
maonyesho Kendraya.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment