Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya
mazungumzo na Mama Denise Nkurunziza,
Mke wa Rais wa Burundi (kushoto) pamoja na Mke wa Rais wa Namibia Mama
Penehupifo Pohamba muda mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe za kukabidhiwa
tuzo za Uongozi Uliotukuka mwiswhoni mwa kikao cha siku tatu cha
wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia kilichofanyika kwenye Hoteli
ya Atlantis The Palm iliyoko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (URA).
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,
Mheshimiwa Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa
(Global Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na
Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa
Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia. Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha
Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD),
wakishirikiana na CEO Clubs Network na African Leadership Magazine uliofanyika
katika hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu
(UAE.)

(UAE.).
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba
ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo
ya Kiuchumi na Uongozi (CELD), Bibi Furo Giami akikabidhi vyeti kwa Wake wa
Marais na wanawake wengine waliotunukiwa tuzo hizo wakati wa kilele cha mkutano
wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliofanyika huko Dubai, Umoja
wa Falme za Kiarabu.
Dr. Angela Moore, Balozi wa Hisani kutoka kutoka
Jimbo la Georgia, nchini Marekani akiwavisha nishani washindi wa Tuzo.
Wake wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha
Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati
walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki
ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya utoaji tuzo hizo
huko Dubai.

Baadhi
ya wajumbe na washiriki waliofuatana na msafara wa Mama Salma Kikwete kwenye
mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wakisherehekea na
kumpongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, wakiongozwa na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Falme za
Kiarabu Mheshimiwa Mbarouk Mbarouk, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Uongozi
Uliotukuka.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao
kwenye sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake
kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliomalizika huko
Dubai, Umoja wa Falme Aza Kiarabu .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao
kwenye sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake
kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliomalizika.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment